NAIBU WAZIRI MAVUNDE AWATAKA WAAJIRI KUHAKIKISHA WAFANYAKAZI WAGENI WANARITHISHA UJUZI KWA WATANZANIA

NAIBU WAZIRI
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana na Ajira Mh Anthony Mavunde akizungumza na wafanyakazi wa  Viwanda vya Sterling Surfancts,A to Z,Nethealth na Polyfoam mkoani Arusha wakati ukaguzi wa viwanda 
  • Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana na Ajira Mh Anthony Mavunde amewataka waajiri wote nchini wenye wafanyakazi wa kigeni kuhakikisha kwamba Wafanyakazi hao wanawarithisha ujuzi Watanzania kwa mujibu wa sheria inavyoelekeza ili kuwajengea uwezo Watanzania na baadaye kutoa nafasi kwa Watanzania kushika nafasi hizo.
NAIBU WAZIRI
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana na Ajira Mh Anthony Mavunde akizungumza na wafanyakazi wa  Viwanda vya Sterling Surfancts,A to Z,Nethealth na Polyfoam mkoani Arusha wakati ukaguzi wa viwanda
  • Mavunde ameyasema hayo mkoani Arusha wakati akifanya ukaguzi katika Viwanda vya Sterling Surfancts,A to Z,Nethealth na Polyfoam mkoani Arusha ambapo alitumia fursa hiyo kuwataka Waajiri kusimamia kifungu cha 7 cha Sheria ya Uratibu wa Ajira kwa Wageni kinachomtaka kila mwajiri kuandaa mpango wa urithishaji wa Ujuzi kwa Wafanyakazi Watanzania kwa lengo la kuhakikisha Watanzania wananufaika na ujuzi huo.
NAIBU WAZIRI
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana na Ajira Mh Anthony Mavunde akizungumza na wafanyakazi wa  Viwanda vya Sterling Surfancts,A to Z,Nethealth na Polyfoam mkoani Arusha wakati ukaguzi wa viwanda 
  • “Kama mwajiri atashindwa kutekeleza matakwa haya ya sheria,hii ni sababu inayojitosheleza kwa mamlaka kutokutoa vibali vya kazi kwa mwajiri mhusika kwa kushindwa kutekeleza Mpango wa Urithishaji Ujuzi”Alisema Mavunde
NAIBU WAZIRI MAVUNDE
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana na Ajira Mh Anthony Mavunde akizungumza na mfanyakazi wa  Viwanda vya Sterling Surfancts,A to Z,Nethealth na Polyfoam mkoani Arusha wakati ukaguzi wa viwanda
  • Wakati huo huo Mavunde alipata nafasi ya kusikiliza kero za Wafanyakazi za kuhusu mikataba na malipo ya muda wa ziada ambapo alitoa maagizo kwa waajiri kuhakikisha ndani ya Siku thelathini(30) wanatatua changamoto hizo.
Ad

Unaweza kuangalia pia

NAIBU WAZIRI SHONZA: WAZAZI NDIYO WALEZI WA KWANZA WA MTOTO

Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza amewataka wazazi na familia kuwa …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *