DKT. MAHIGA AZINDUA KAMPENI YA USAJILI NA UTOAJI VYETI VYA KUZALIWA KWA WATOTO CHINI YA MIAKA MITANO

  • Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga amezindua kampeni ya usajili wa watoto chini ya miaka mitano na kuwapatia vyeti vya kuzaliwa kwa mikoa ya Dodoma na Singida.
WAZIRI WA KATIBA
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akionyesha kitabu kinachotumika kusajili watoto chini ya miaka mitano na kuwapatia vyeti vya kuzaliwa baada ya kuzindua kampeni ya usajili wa watoto chini ya miaka mitano na kuwapatia vyeti vya kuzaliwa kwa mikoa ya Singida na Dodomajini Singida
  • Akizindua kampeni hiyo, Dkt. Mahiga ameitaka RITA kuhakikisha  inatunza taarifa za watoto wanazozichukua kupitia mtandao wa simu  na kuhakikisha  zinapatikana pale zitakapohitajika.
  • “Kuwasajili watoto hawa kwa kasi hii ni vizuri lakini kazi kubwa  ni kuhakikisha taarifa hizo zinawekwa na kutunzwa kule zinakostahili na zinapatikana wakati wote”, alisema Dkt Mahiga.
PICHA YA PAMOJA
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akiwa katika picha ya pamoja na wananchi mbalibali , wazazi na watoto waliopata vyeti vya kuzaliwa na watendaji wa RITA baada ya kuzindua usajili wa watoto kwa mikoa ya Singida na Dodoma katika viwanja vya stendi mjini Singida
  • Amesema Serikali itaendelea kulinda haki za msingi za raia wake na ndio maana umeamua kutekeleza mpango wa Usajili na utoaji vyeti vya kuzaliwa kwa watoto chini ya miaka mitano kwa kuwa cheti cha kuzaliwa ni haki ya kila mtoto.
  • Amesema cheti cha kuzaliwa ni alama na vitambulisho wa uraia wa kila mtu na kwamba Tanzania imeamua raia wake wote wawe na utambulisho wao.
  • Akizungumza katika uzinduzi huo Mtendaji Mkuu wa RITA bibi Emmy Hudson amesema tangu kuanza kwa awamu ya kwanza ya kampeni hiyo  jumla ya watoto milioni tatu wamesajiliwa na kupewa vyeti katika mikoa ya Mbeya, Mwanza, Simiyu, Geita, Njombe, Iringa, Songwe, Mara, Musoma, Lindi, Mtwara, Dodoma na Singida na inakadiriwa hadi kampeni hiyo itakapokamilika mwisho ni mwa mwezi huu zaidi ya watoto milioni tatu na nusu watakuwa wamesajiliwa.
WAZIRI WA KATIBA
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akimkabidhi mzazi wa mtoto aliesajiliwa na kupata cheti cha kuzaliwa katika viwanja vya stand mjini Singida
  • Awali akizungumza katika uzinduzi huo Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe. Dkt. Rehema Nchimbi aliahidi kukusimamia Mkoa wa Singida ili uweze kufanya usajili kwa watoto zaidi ya lengo lililorekebishwa la watoto 280,000 ndani ya wiki mbili ambapo alisema hadi kufikia Machi 20 mkoa wake ulikuwa umesajili zaidi ya  watoto 180,000
  • Kazi ya usajili wa watoto hao inafanywa na wasajili wasaidizi ambao wamepewa Mafunzo maalum ya kuingiza taarifa za watoto kwa kutumia simu ya Mkononi na  inafanyika katika vituo vyote vya afya na  katika ofisi za kata ili kuwafikia wananchi wengi zaidi.
  • Uzinduzi huo umefanyika katika viwanja vya stendi mjini Singida na kuhudhuriwa na viongozi na watendaji wa serikali kutoka mikoa ya Singida na Dodoma wadau wa maendeleo wa UNICEF, CANADA na kampuni ya TIGO ambayo imetoa simu na mtandao wa simu wake unaothmika kufanya usajili wa watoto katika mikoa hiyo nchini.
Ad

Unaweza kuangalia pia

NCHI ZA SADC ZATAKIWA KUTATHMINI UCHUMI WAKE BILA KUTEGEMEA MASHIRIKA YA KIMATAIFA PEKEE

Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango amesema kuwa nchi za Afrika hasa zilizopo …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.