Naibu Waziriwa Ujenzi, Elias Kwandikwa, amemtaka mkandarasi anayejenga daraja la mfuto (drift) katika mto Nguyami linalounganisha kijiji cha Iyogwe na Gairo kuongeza kasi ya ujenzi ili kuwaondolea kero wananchi wa eneo hilo.
Akizungumza na wananchi wa vijiji hivyo mara baada ya kukagua barabara ya Iyogwe-Chakwale-Ngilori yenye urefu wa KM 42, wilayani Gairo, Naibu Waziri amesema Serikali imejipanga kuhakikisha madaraja 3 katika barabara hiyo yanakamilika na hivyo kuwezesha shughuli za kiuchumi na uzalishaji kwa wakazi wa eneo hilo.