RC HOMERA AZINDUA MRADI WA MAJI CHAMALENDI, KATAVI

  • Mkuu wa mkoa wa Katavi Juma Zuberi Homera tarehe 11.07.2019 amezindua mradi wa maji katika kijiji cha Chamalendi kata ya Chamalendi Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe wilayani Mlele.

MJ 2-01

  • Mradi huo wenye thamani ya Tsh 402,600,000/=  umeshuhudiwa na wananchi wa eneo hilo ambapo mradi huu utahudumia wananchi zaidi ya 10,000 Katika kata hiyo ya chamalendi.
MJ 3-01
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Juma Homera akifungua maji
  • Mkuu wa mkoa Homera amempongeza waziri wa Maji Prof Makame Mnyaa Mbarawa kwa usimamizi wa karibu wa miradi ya maji mkoani Katavi na kupelekea kutekelezwa kwa asilimia zaidi ya 99.
  • Mkuu wa wilaya hiyo ya Mlele Mhe. Rachel Kasanda amewataka wananchi hao kuutunza Mradi huo kwa kutumia vyema fedha za michango ya watumia maji ili mabomba yakiharibika waweze kukarabati na kuongeza vioski vingine vya kuchotea maji kutoka 20 na kuongeza vingine zaidi.
Ad

Unaweza kuangalia pia

WAKAZI WA KIGWA KUPATA MAJI KUTOKA ZIWA VICTORIA KWA GHARAMA YA BILIONI 10

Serikali imeamua kupeleka maji katika Kata ya Kigwa wilayani Uyui kupitia mradi wa ujenzi wa …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *