WAJUMBE WA BODI ZANZIBAR WAIPONGEZA MLOGANZILA

  • Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila- imewekea mikakati mbalimbali ya kuhakikisha inaendelea kutoa huduma bora za afya kwa wananchi ikiwemo huduma za kibingwa na kibobezi.
ML 4-01
Kiongozi kutoka kitengo cha usafishaji damu MNH-Mloganzila Nurdin Mtumbuka (aliyesimama katikati) akiwaeleza viongozi wa Hospitali ya Mmnazi Mmoja kuhusu utoaji wa huduma ambapo kitengo hicho kina uwezo wa kuhudumia wagonjwa 36 kwa siku.
  • Hayo yamesemwa leo jijini Dar es salaam na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Muhimbili-Mloganzila Dkt. Julieth Magandi wakati akizungumza na viongozi wa Hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar ambao wamefanya ziara ya siku moja katika Hospitali ya Mloganzila kwa lengo la kujifunza muonekano na upangaji wa huduma katika hospitali za kisasa.
ML 6-01
Baadhi ya viongozi wa Hospitali ya Mloganzila na Mmnazi Mmoja Zanzibar, wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumaliza kutembelea maeneo mbalimbali ya hospitali hii leo.
  • Ujumbe wa viongozi hao umeongozwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Hospitali hiyo Dkt. Abdulwakil Idrisa Abdulwakil.
ML 2-01
Viongozi wa Hospitali ya Mmnazi Mmoja Zanzibar wakiwa katika mkutano kabla ya kuanza kutembelea maeneo mbalimbali ya Hospitali.
  • Dkt. Magandi amesema dhamira ya hospitali ni kuwawezesha wananchi wengi kupata huduma za kibingwa sambamba na kuunga mkono juhudi za serikali za kupunguza rufaa za wagonjwa kwenda kutibiwa nje ya nchi.
ML 1-01
Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Muhimbili-Mloganzila Dkt. Julieth Magandi (kulia) akizungumza na viongozi wa Hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar ambao leo wametembelea Hospitali ya Mloganzila kwa lengo la kujifunza muonekano na upangaji wa huduma katika hospitali za kisasa. Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Mnazi Mmoja Dkt. Abdulwakil Idrisa Abdulwakil.
  • Pia amesema idadi ya wagonjwa katika Hospitali ya Mloganzila inaendelea kuongezeka ambapo katika kipindi cha Oktoba mwaka jana wagonjwa wa nje walikua takribani 200 kwa siku lakini kwa sasa wanafikia wagonjwa 500 kwa siku huku wagonjwa wa ndani wakiongezeka kutoka 100 mpaka zaidi ya 300.
ML 3-01
Kaimu Mkurugenzi wa Ufundi MNH- Mloganzila Mhandisi Andrew Fungamali (katikati) akielezea kuhusu mfumo wa maji na mfumo wa kuzima moto unavyofanya kazi.
  • Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Hospitali ya Mnazi Mmoja Dkt. Abdulwakil Idrisa Abdulwakil ameshukuru ushirikiano uliopo na kueleza kuwa Hospitali ya Mloganzila na Mnazi Mmoja wamekuwa na ushirikiano wa karibu wa kubadilishana uzoefu katika maeneo mbalimbali ikiwemo huduma ya kusafisha damu na huduma ya mama na mtoto.
Ad

Unaweza kuangalia pia

RAIS DKT. SHEIN AWAAPISHA VIONGOZI ALIOWATEUA

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein  amewaapisha viongozi …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *