RAIS MAGUFULI APOKEA DHAHABU YA TANZANIA ILIYOKAMTWA NCHINI KENYA MWAKA 2018

  • Rais Dkt. John Magufuli aipongeza Serikali ya Kenya kwa maamuzi yake ya kuirejeshea dhahabu zenye uzito wa kilo 35.34 zilizotoroshwa nchini Tanzania na Wafanyabiashara wasio waamini kwa njia ya magendo mwaka 2018.
FM 6-01
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akisaidia kuhesabu vipande vya dhahabu huku akishuhudiwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba Kabudi aliyevipokea kutoka kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya Mhe. Balozi Monica Juma Dhahabu pamoja na pesa zilizokamatwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi zikitoroshwa kutoka Tanzania kwenye hafla ya makabidhiano iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumanne Julai 24, 2019.
  • Akizungumza katika hafla ya kukabidhi dhahabu pamoja na fedha taslimu akiwa pamoja na ujumbe wa Mawaziri na Watendaji wa Serikali ya Kenya leo Jumatano (Julai 24, 2019) Ikulu Jijini Dar es Salaam, Rais Magufuli amesema kitendo kilichofanywa na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ni cha kizalendo na kimedhirisha urafiki na undugu wa kweli baina yake na Tanzania.
FM 5-01
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akisaidia kuhesabu vipande vya dhahabu huku akishuhudiwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba Kabudi aliyevipokea kutoka kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya Mhe. Balozi Monica Juma Dhahabu pamoja na pesa zilizokamatwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi zikitoroshwa kutoka Tanzania kwenye hafla ya makabidhiano iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumanne Julai 24, 2019.
  • Amesema kuwa  Serikali ya Kenya kupita vya vyombo ulinzi na usalama vimefanya kazi nzuri inayodhirisha ushirikiano uliopo  kati ya Tanzania na Kenya,  na ameeleza kuwa  kama kusingekuwepo na ushirikiano huo dhahabu na pesa  hizo zilizokamatwa kwenye uwanja wa Jommo Kenyatta nchini humo visingelejeshwa Tanzania.
  • “Tunaipongeza  Serikali ya Kenya kupitia vyombo vya vyake vya ulinzi vilivyofanya kazi nzuri ya kukamata dhahabu kilo 35.34 iliyokuwa imeshavuka kwenye mipaka yetu, na  tuwapongeze pia kwa kutunza pesa yetu ambayo ilibiwa Tanzania kwenye Benki ya NMB mwaka 2004, kwa kweli huu ni uaminifu mkubwa” amesema Rais Magufuli
  • Licha ya kuipongeza vyombo vya ulinzi vya Kenya Rais Magufuli ameshangazwa na ukimya  kutaka vyombo vya ulinzi vya Tanzania na hivyo kuvitaka kujitafakari kwa namna dhahabu hiyo ilivyoweza kukamatiwa  Kenya na Sio Kwenye uwanja wa ndege wa Mwanza  ambapo watuhumiwa walitumia ndege ya ‘Precision Air’ kusafirisha mzigo huo.
  •  “Vyombo vyetu vya ulinzi vipo hapa lazima niviseme, dhahabu iliwezaje kufika Kenya tukashindwa kuwakamata watumiwa wakiwa bado kwenye uwanja wa Mwanza?, hapa lazima vyombo vyetu mjitafakari japo mnafanya kazi kubwa lakini ikiwezekana mkajifunze kwa wenzenu wawape mbinu walizozitumia katika hili” amesema Rais Magufuli.
FM 4-01
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akishuhudia Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba Kabudi akipokea kutoka kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya Mhe. Balozi Monica Juma Dhahabu pamoja na pesa iliyokamatwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi zikitoroshwa kutoka Tanzania kwenye hafla ya makabidhiano iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumanne Julai 24, 2019
  • Katika hafla hiyo, Rais Magufuli pia  alimpigia simu ya moja kwa moja Rais Uhuru Kenyatta na kutoa shukrani zake na kumdhibitishia kuwa amepokea mzigo huo na kumpongeza kwa ushirikiano wa Serikali yake kwa Watanzania, ambapo Rais Kenyatta akimuhakikishia Rais Magufuli ushirikiano wa kudumu ambao utachochea zaidi maendeleo kama walivyohaidi na kupewa mamlaka na wananchi.
  • Naye mjumbe maalumu aliyemwakilisha Rais Kenyatta, Monica Juma ambaye ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Serikali ya Kenya amesema Serikali ya Kenya itaendeleza ushirikiano wake na  Tanzania katika masuala ya ulinzi na usalama kwa kuwa ushirikiano huo utasaidia kukuza uchumi wa pande zote mbili.
FM 3-01
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan akisalimiana kwa simu ya mkononi na Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe Jomo Kenyatta baada ya viongozi hao kushuhudia Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba Kabudi akipokewa kutoka kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya Mhe. Balozi Monica Juma Dhahabu pamoja na pesa iliyokamatwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi zikitoroshwa kutoka Tanzania kwenye hafla ya makabidhiano iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumanne Julai 24, 2019. Kushoto ni Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan akifuatiwa na Mhe Monica Juma. Kutoka kulia ni Waziri wa Madini Mhe. Dotto Biteko akifuatiwa na Profesa Kabudi na Mwendesha Mashataka Mkuu wa Serikali Mhe Biswalo Mgangha
  • Na kwa upande wake Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Palamagamba Kabudi amesema Kenya na Tanzania ni ndugu tokea ezi na enzi, hivyo Serikali Tanzania itahakikisha kuwa inaendelea kushirikiana na Kenya ili kufanya ushirikiano huo unaleta manufaa kwa wananchi wa nchi hizo.
Ad

Unaweza kuangalia pia

NAIBU WAZIRI MAMBO YA NJE DKT. NDUMBARO AMEKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA MABALOZI WA NCHI TANO HAPA NCHINI

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *