SHILINGI TRILIONI 18 ZINAPITA KWENYE HUDUMA YA FEDHA MTANDAO KWA MWEZI

Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Faustine Ndugulile akifafanua jambo kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu wakati wa kikao chake na wajumbe wa Kamati hiyo Bungeni, Dodoma. Wa pili kushoto aliyeketi ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mhandisi Kundo Mathew na wa tatu kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Zainab Chaula

Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Faustine Ndugulile ameiarifu Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu kuwa kiasi cha shilingi trilioni 18 zinapita kwenye mitandao kwa mwezi wakati wa kikao chake na kamati hiyo kilichohudhuriwa na wajumbe wa Menejimenti ya Wizara hiyo na wakuu wa taasisi zake ikiwemo Shirika la Posta Tanzania (TPC), Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), Baraza la Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano (TCRA -CCC) na Tume ya TEHAMA (ICTC) kilichofanyika kwenye ukumbi wa Bunge, Dodoma

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Moshi Kakoso (wa tatu kushoto aliyeketi) akiwa kwenye picha ya pamoja na Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Faustine Ndugulile (wa tatu kulia), Naibu Waziri, Mhandisi Kundo Mathew (wa pili kulia) na Katibu Mkuu, Dkt. Zainab Chaula (wa pili kushoto) na wajumbe wa Kamati hiyo waliosimama mbele ya banda la TTCL baada ya kikao chao Bungeni, Dodoma

Dkt. Ndugulile amewaeleza wajumbe wa Kamati hiyo kuwa kiasi cha miamala milioni 300 inafanyika kwa mwezi mtandaoni na Serikali inapata shilingi bilioni 80 kwa mwezi za tozo kutokana na fedha zinazopita mtandaoni na mzunguko huo wa fedha mtandaoni kwa mwezi, miamala inayofanyika na tozo ambazo Serikali inapata ni kutokana na kuwepo kwa matumizi ya TEHAMA

Amefafanua kuwa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano ni njia kuu ya uchumi na inawezesha upatikanaji wa huduma za mawasiliano yenye kasi, kufanikisha utendaji kazi wa mifumo ya TEHAMA na huduma za fedha mtandaoni ambapo Wizara imejipanga kuandaa ramani ya njia ya  miundombinu huo ili kufanikisha mwingiliano wa ujenzi na upanuzi wake pale inapokutana na njia za miundombinu mingine kama vile ya barabara, maji, umeme na reli

Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhandisi Kundo Mathew akifafanua huduma zinazotolewa na Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) kwa mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Ritta Kabati (aliyesimama katikati) kwenye viwanja vya Bunge, Dodoma baada ya kikao cha Wizara hiyo na wajumbe wa Kamati hiyo. Kushoto ni Meneja wa T-PESA, Lulu Mkude
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Anne Kilango Malecela (wa kwanza kushoto) na wajumbe wa Kamati hiyo wakifurahia jambo wakati Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Faustine Ndugulile (hayupo pichani) akifafanua jambo kwa Kamati hiyo alipowasilisha taarifa ya majukumu ya Wizara yake Bungeni, Dodoma
 

Naye Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Moshi Kakoso ameitaka Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kuongeza udhibiti na usimamizi wa huduma za mawasiliano kwenye suala la fedha mtandao ili kudhibiti mianya ya upotevu wa fedha na kuweza kuongeza mchango wa tozo Serikalini zaidi ya shilingi bilioni 80 kwa mwezi kwa kuwa miamala mingi ya fedha inafanyika na fedha nyingi zinapita kwenye mtandao ili TEHAMA iongeze mchango wake kwenye ukuaji wa uchumi na kuchangia zaidi pato la taifa

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Moshi Kakoso (wa tatu kushoto aliyeketi) akiwa kwenye picha ya pamoja na Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Faustine Ndugulile (wa tatu kulia) na wakuu wa taasisi za Wizara hiyo waliosimama mbele ya banda la TTCL baada ya kikao chao Bungeni, Dodoma. Wa pili kushoto ni Naibu Waziri, Mhandisi Kundo Mathew na wa pili kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Zainab Chaula

Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mhandisi Kundo Mathew amesema kuwa Wizara itaipa ushirikiano wa kutosha Kamati hiyo ili kwa pamoja Serikali kupitia Wizara hii na Bunge kupitia Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu waweze kutekeleza majukumu yao kwa kuwa wote kwa pamoja wanamhudumia mwananchi

Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Zainab Chaula amewaeleza wajumbe wa Kamati hiyo kuwa Wizara itaendelea kusimamia na kuendesha vema Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano ili kuhakikisha kuwa wananchi wanaendelea kunufaika na huduma za mawasiliano na TEHAMA inatumika kurahisisha maisha yao ya kila siku katika nyanja ya kiuchumi na kijamii

Unaweza kuangalia pia

RAIS SAMIA AMEDHAMIRIA KUMSHUSHA MAMA NDOO KICHWANI – MAJALIWA

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amemuagiza Meneja wa RUWASA Wilaya ya Kilwa, kufanya utafiti wa kina …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.