CHUO CHA UHASIBU ARUSHA CHASAINI MKATABA NA TFF KUENDELEZA SOKA NCHINI.

Na: Eleuteri Mangi- WHUSM, Arusha.

Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) kimesaini mkataba wa makubaliano ya ushirikiano na Shirikisho la Soka nchini (TFF) ili kuendelea kukuza michezo nchini.

Ad
Rais wa TFF Wales Karia Kushoto na Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Arusha Prof. Eliamani Sedoyeka Kulia Wakionesha Mkataba wa Ushirikiano Waliosaini Kuendeleza Mchezo wa Soka Baina ya Taasisi Hizo Januari 27 Jijini Arusha.

Akizunzungumza mara baada ya utiwaji wa saini makubaliano hayo Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa amepongeza hatua hiyo ya Chuo cha Uhasibu Arusha kuunganisha taaluma na sekta ya michezo hatua inayosaidia kulea, kukuza na kuendeleza vipaji katika michezo mbalimbali.

Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) Prof. Eliamani Sedoyeka (wa tatiu kulia) Akitoa Maelezo kwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa alipotembelea ,maeneo mbalimbali ya Chuo Hicho Januari 27 Jijini Arusha

“Tutakitumia chuo hiki kama mfano kwa kufanikiwa kuunganisha mnyororo wa thamani kati ya taaluma na michezo, hatua hii ni mfano wa kuigwa na vyuo vingine nchini ili kiuandaa wanataaliuma na wanamichezo ambao wataleta tija kwa taifa kwa kujiongezea vipato vyao na pato la taifa” alisema waziri Bashungwa.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo  Mhe. Innocent Bashungwa akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Chuo cha  Uhasibu  Arusha (IAA) Pamoja na Viongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF Mara Baada ya Kusaini Makubaliano ya ushirikiano Katika Kundeleza Soka Nchini leo Januari 27 Jijini Arusha

Awali akiongea katika hafla hiyo fupi ya utiwaji wa saini ya makubaliano hayo Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Arusha Prof. Eliamani Sedoyeka alisema hatua hiyo ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika kuendeleza mitaala ya michezo hususan somo la uongozi wa soka kwa ngazi ya Cheti, Astashahada, Stashahada, Shahada na Shahada ya Uzamili na hatimae hatiua ambayo itasaidia katika uanzishaji na uendeshaji wa shule ya uongozi wa soka.

Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) Prof. Eliamani Sedoyeka (wa tatiu kulia) Akitoa Maelezo kwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa alipotembelea ,maeneo mbalimbali ya Chuo Hicho Januari 27 Jijini Arusha

“Mwaka ujao wa masomo wa 2021/2022, tumepanga kutoa ufadhili wa masomo kwa vijana watakaofanya vizuri katika soka, na TFF watatusaidia katika kuwapata vijana hao, chuo kitawapa ufadhiri wa masomo kwa upande wa ada na malazi” alisema Prof. Sedoyeka.

Kwa upande wake Rais wa Shirikisho la Soka nchini TFF Wales Karia alisema mkakati huo wa chuo cha Uhasibu Arusha ni jawabu la kusimamia na kuendeleza wanamichezo ambao walikuwa wanapotea baada ya kumaliza kidato cha nne au cha Sita.

Ad

Unaweza kuangalia pia

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Isdory Mpango, tarehe 01 Novemba 2024 ameungana na kuongoza Waombolezaji Katika Hospitali Kuu ya Jeshi Lugalo,jijini Dar-es-Salaam, kuaga mwili wa marehemu Mkuu wa Majeshi Mstaafu Jenerali David Bugozi Musuguri

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *