WAZIRI MWAMBE AFANYA MAZUNGUMZO NA MTENDAJI MKUU WA DANGOTE PAMOJA NA WAZALISHAJI WA SUKARI NCHINI

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Geoffrey Mwambe,akiwa katika picha ya pamoja na Mtendaji Mkuu na Meneja wa kiwanda cha Dangote nchini Tanzania Bw.Abdullahi Baba mara baada ya mazungumzo ofisini kwake leo Januari 29,2021 jijini Dodoma

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Geoffrey Mwambe, amekutana na wazalishaji wa Sukari nchini na kusikiliza changamoto zao ili kuzitatua na kuongeza uzalishaji na kuhakikisha Sukari inapatikana kwa urahisi wakati wote nchini.

Akizungumza na na wazalishaji hao leo Janauari 29,2021 jijini Dodoma Mhe. Mwambe amesema kuwa Serikali inalenga kuongeza uzalishaji wenye tija  kwa kutumia teknlojia na miundombinu ya kisasa ya umwangiliaji.

Ad
Waziri wa Viwanda na Biashara Geoffrey Mwambe akiongoza kikao

”Leo nimekutana na nyie kwa leongo la kujifunza na kujua changamoto mlizonazo katika uzalishaji wa sukari nchini na waahidi tutazifanyia kazi”amesema Mhe.Mwambe.

Hata hivyo Mhe.Mwambe amewatoa wasiwasi wazalishaji hao kuwa Serikali itashughulikia changamoto hizo ili  kuleta maendeleo na kuongeza uzalishaji zaidi nchini .

Awali Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Geoffrey Mwambe,amekutana na kufanya mazungumzo na Mtendaji Mkuu na Meneja wa kiwanda cha Dangote nchini Tanzania Bw.Abdullahi Baba.

Ad

Unaweza kuangalia pia

Mitazamo ya Uongozi ya Mhe. Ummy Ally Mwalimu katika Sekta za Afya, Maendeleo ya Jamii, na Haki za Watoto

Ummy Ally Mwalimu ameonyesha mitazamo ya uongozi yenye mwelekeo wa kujali maendeleo na ustawi katika …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *