RAIS DKT. MWINYI ASHUHUDIA UTIAJI SAINI MAELEWANO (MoU) UJENZI WA BANDARI MANGAPWANI NA MJI WA KISASA BUMBWINI ZANZIBAR

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akizungumza baada ya kumalizika utiaji wa Saini Hati ya Maelewano (MoU)  ya ujenzi wa Bandari ya Mwangapwani na ujenzi wa Mji wa Kisasa Bumbwini Zanzibar, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdulla, Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said, Mwanasheria Mkuu Zanzibar.Dkt. Mwinyi Talib Haji na Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi Mhe.Rahma Kassim Ali, wakifuatilia hutub ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi, baada ya kumalizika zoezi la utiaji wa saini ya maelewano ya Ujenzi wa Bandari Mangapwani na Mji wa Kisasa Bumbwini Zanzibar, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu)
Baadhi ya Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar wakifuatilia hutuba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) baada ya kumalizika kwa utiaji wa Saini ya Hati ya Maelewano (MoU) kuhusu Mpango Mkuu”Master Plan “ ya Ujenzi wa Bandari na Mji wa Kisasa Mangapwani  na Bumbwini Zanzibar, hafla hiyo imefanyika katika ukumbin wa Ikulu Jijini Zanzibar.
Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar Mhe.Rahma Kassim  Ali, akizungumza wakati wa Utiaji Saini ya Maelewano (MoU) kuhusu Mpango Mkuu wa Ujenzi wa Bandari na Mji wa Kisasa Mangapwani na Bumbwini Zanzibar, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo 28-1-2021.
Mkurugenzi Mkuu wa Oman Investment Authority  (OIA) Bw. Sheikh Mohammed Al Taooqi, akizungunza kabla ya kutowa maelezo mafupi ya Ujenzi wa Bandari na Mji wa Kisasa Mangapwani na Bumbwini Zanzibar, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.

Unaweza kuangalia pia

RAIS SAMIA AMEDHAMIRIA KUMSHUSHA MAMA NDOO KICHWANI – MAJALIWA

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amemuagiza Meneja wa RUWASA Wilaya ya Kilwa, kufanya utafiti wa kina …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.