HALMASHAURI YA CHALINZE MKOANI PWANI YATEKELEZA MAAGIZO YA WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA

Halmashauri ya Chalinze mkoani Pwani imetekeleza maagizo ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kwa kutengeza madawati 355, meza na viti 221, huku Mbunge wa Jimbo hilo Ridhiwani Kikwete akichangia shilingi milioni 3.67.

Akizungumza wakati wa kupokea madawati hayo zoezi lilofanyika Mioni Wilayani Bagamoyo, Mbunge Kikwete amesema kuwa madawati hayo ni kwaajili ya shule 38, ambapo za sekondari 20 na shule za msingi 18.

Ad

Kikwete amesema kuwa lengo ni kuhakikisha hakuna mwananfunzi anayekaa chini “lengo letu ni kuona wanafunzi wote wanakaa kwenye madawati ili waweze kuandika vizuri wanapokuwa darasani na kuacha kukaa chini darasani” Amesema Kikwete

Madawati hayo yamepokelewa mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani Evarist Ndikilo na Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Bi Zainab Kawawa.

Ad

Unaweza kuangalia pia

Serikali ya Tanzania na Czech Zakubaliana Kuondoa Utozaji Kodi Mara Mbili

Serikali za Tanzania na Czech kukuza ushirikiano wa kiuchumi na kuvutia uwekezaji kati yao. Kuondoa …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *