- Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, ametembelea Shirika la Viwango Tanzania (TBS) ili kujionea utendaji kazi wa shirika hilo.
Waziri Mkuu Majaliwa alifanya ziara hiyo jana Makao Makuu ya Shirika jijini Dar es Salaam akiwa ameongozana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji), Angella Kairuki, Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia,Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhandisi Stella Manyanya.
- Waziri Mkuu alitoa pongezi kwa kazi nzuri inayofanywa na Shirika la Viwango Tanzania na kwamba ameridhishwa na utendaji wa kazi pamoja na kuwepo kwa vifaa vya kisasa na wataalam wazuri katika maabara zake. “Nimefurahishwa na utendaji kazi wenu pamoja kuwepo kwa vifaa vya kisasa vya maabara pamoja na wataalamu,” alisema.
- Waziri Mkuu Majaliwa aliielekeza TBS kufanya kazi kwa weledi kwa kuhakikisha inakuwa na maofisa kila mkoa na wilaya ili kuweza kusogeza huduma karibu zaidi kwa wananchi.
- Alitoa mwito kwa wafanyakazi wa TBS kuendelea kufanya kazi kwa weledi na juhudi na kuhakikisha umma wanaelimishwa zaidi kuhusiana na shughuli zinazofanywa na shirika hilo hapa nchini.
- Wakati huo huo, Waziri Mkuu Majaliwa aliwataka Mawaziri wa Kilimo, Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Mifugo na Uvuvi na Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto wakutane na wafanye mapitio ya taasis zao na kuangalia maeneo yanayogongana kiutendaji ili kila mmoja abaki na jukumu lake.
- Aliagiza apelekewe taarifa za mapendekezo hayo ifikapo Machi 30,2019. Alifikia uamuzi huo baada ya kuwepo kwa malalamiko kutoka kwa baadhi ya wafanyabiashara ambao wamedai kuwepo kwa muingiliano wa majukumu ya kiutendaji wa taasis hizo.
- “Kutaneni pitieni maelekezo ya Serikali yanayoelekeza namna ya kuzifanya taasisi hizi na zingine zinazofanya shughuli zinazofanana zilizo katika wizara zenu bila kusahau Mpango wa Kuboresha Mazingira ya Biashara (blue print). Ifikapo tarehe 30 mwezi huu niwe nimepata mapendekezo yenu,” alisisitiza.
Ad