Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia kwenye mkutano wa Africa Now Summit 2019 ulioanza leo kwenye hoteli ya Commonwealth Resort, Munyonyo jijini Kampala, Uganda.

MKUTANO WA AFRICA NOW SUMMIT 2019 WAFUNGULIWA KAMPALA NCHINI UGANDA

Rais wa Uganda
Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni akihutubia wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Africa Now Summit 2019 ambapo viongozi wa Afrika wanakutana kujadili masuala mbalimbali ya utengamano katika kuleta maendeleo endelevu barani Afrika ambapo Tanzania imewakilishwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.
  • Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema ili kuibadili Afrika Viongozi wake lazima wawekeze kwa Vijana na Watoto.
  • Makamu wa Rais ameyasema hayo  wakati akihutubia kwenye mkutano wa Africa Now Summit 2019 jijini Kampala nchini Uganda.
MAKAMU WA RAIS
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (kushoto) akiwa na mwenyeji wa Mkutano wa Africa Now Summit 2019 Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni pamoja na Rais wa Somalia Mhe. Mohamed Abdullahi Mohamed (kulia) wakati wakielekea kwenye ukumbi wa mkutano katika hoteli ya Commonwealth Resort, Munyonyo jijini Kampala Uganda.
  • “Viongozi lazima wahakikishe wanawekeza kwenye lishe bora ya watoto wanaozaliwa na kuhakikisha mifumo yetu ya elimu inalenga katika kutoa elimu bora na zenye kukuza vipaji ili kwenda sawa na ulimwengu wa teknolojia.”alisema Makamu wa Rais.
  • Aidha Makamu wa Rais amesisitiza Afrika lazima iwekeze kwenye mipango itakayoleta maendeleo endelevu kwa vizazi vijavyo na si mipango kwa ajili ya chaguzi zijazo.
MAKAMU W ARAIS
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (kushoto) akiwa na mwenyeji wa Mkutano wa Africa Now Summit 2019 Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni pamoja na Rais wa Somalia Mhe. Mohamed Abdullahi Mohamed (kulia) wakati wakielekea kwenye ukumbi wa mkutano katika hoteli ya Commonwealth Resort, Munyonyo jijini Kampala Uganda.
  • Mkutano huo uliofunguliwa na Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni unalengo la kuwakutanisha Viongozi wa Afrika kujadili masuala mbalimbali ya utengamano katika kuleta maendeleo endelevu barani Afrika.
Rais wa Uganda
Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni akihutubia wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Africa Now Summit 2019 ambapo viongozi wa Afrika wanakutana kujadili masuala mbalimbali ya utengamano katika kuleta maendeleo endelevu barani Afrika ambapo Tanzania imewakilishwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.
  • Rais Museveni amesema kwa kipindi kirefu Afrika haijabadilika ni wakati wa kuboresha elimu, kuboresha bidhaa zinazoingia sokoni, kupanua soko la kimataifa ambalo kwa sasa limeonekana finyu na kuimarisha miundombinu na kutambua umuhimu wa Sekta Binafsi katika kuleta mabadiliko endelevu ya kiuchumi.
MAKAMU WA RAIS
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia kwenye mkutano wa Africa Now Summit 2019 ulioanza kwenye hoteli ya Commonwealth Resort, Munyonyo jijini Kampala, Uganda.
  • Viongozi wengine walioshiriki wakati wa ufunguzi ni Rais wa Somalia Mhe. Mohamed Abdullahi Mohamed, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, Naibu Rais wa Kenya Mhe. William Ruto na Waziri wa Biashara na Viwanda wa Misri Mhe. Amr Nassar.
Makamu wa Rais
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Miss Uganda 2018 ambaye pia ni Miss World Africa Quiin Abenakyo (kulia) wakati wa mkutano wa Africa Now Summit 2019 unaofanyika Munyonyo, mjini Kampala, Uganda.
Ad

Unaweza kuangalia pia

SERIKALI KUENDELEA KUCHUKUA HATUA KWA WAZALISHAJI NA WASAMBAZAJI WA MIFUKO ISIYOKIDHI VIWANGO – WAZIRI ZUNGU

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Azzan Zungu …

Oni moja

  1. privanus katinhila

    Hongera sana kwa Makamu wetu wa Rais wetu kushiriki katika kikao hiki muhimu sana kwa maendeleo ya Taifa letu na watu wake
    hongera sana

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *