WAZIRI WA FEDHA – UJENZI WA SGR UNAENDELEA VIZURI KAMA ULIVYOPANGWA

  • Waziri Fedha na MIpango Dr Philip Mpango amesema Ujenzi wa Reli ya Kati kwa kiwango cha Standard Gauge: Ujenzi wa kipande cha Dar es Salaam – Morogoro (km 300) unaendelea vizuri kama ilivyopangwa, ambapo shughuli zinazoendelea ni ujenzi wa madaraja, makalavati, daraja lenye urefu wa km 2.54 katikati ya jiji la Dar es Salaam, ukataji wa miinuko, ujazaji wa mabonde na utandikaji wa reli.
  • Aidha amesema katika kipande cha Morogoro – Makutupora (km 422), kazi zinazoendelea ni pamoja na ukataji wa miinuko na ujazaji wa mabonde, usanifu wa njia na ujenzi wa kambi za Kilosa na Ihumwa.
  • Kwa upande wa kipande cha Isaka – Rusumo (km 371), hatua iliyofikiwa ni kukamilika kwa mapitio ya upembuzi yakinifu na usanifu wa awali wa njia ya reli.
  • Aidha, taratibu za ununuzi wa mabehewa, injini na mitambo itakayotumika kutoa huduma ya usafiri kwenye reli ya Standard Gauge zipo katika hatua za mwisho.
  • Katika miradi inayogharamiwa na mfuko wa reli, shughuli zilizofanyika ni:
  • kununua vichwa 11 vya treni kwa ajili reli ya kati; kuendelea na ukarabati wa reli ya Tanga – Arusha (km 439) ambapo kipande cha Tanga – Mombo (km 129) kimeanza kufanya kazi ya kusafirisha mizigo na ukarabati wa vipande vya Mombo – Same (km124) na Same – Arusha (km 186) unaendelea. Aidha, kazi ya ukarabati wa mabehewa inaendelea ambapo hatua iliyofikiwa ni kukamilika kwa ukarabati wa mabehewa 15.
Ad

Unaweza kuangalia pia

NCHI ZA SADC ZATAKIWA KUTATHMINI UCHUMI WAKE BILA KUTEGEMEA MASHIRIKA YA KIMATAIFA PEKEE

Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango amesema kuwa nchi za Afrika hasa zilizopo …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *