TANZANIA YAPATA HESHIMA KWENYE MKUTANO WA SOUTH – SOUTH COOPERATIONS, BUENOS AIRES, ARGENTINA.

  • Tanzania imesifiwa na Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayoshughulikia Uhusiano wa Nchi za Kusini (UNOSSC) , Umoja wa nchi Afrika, Karibian na Pasifiki (ACP) pamoja na nchi mbalimbali kwa namna ambavyo inapambana kulinda rasimali zake za asili na kudhibiti utoroshaji haramu wa fedha toka Afrika kwenda kwenye nchi zilizoendelea.
  • Akiwasilisha mada kuhusu juhudi za Tanzania katika eneo hilo Mh . Dkt Damas Ndumbaro, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, alieleza mafanikio hayo ni matokeo ya utashi wa kisaisa ambayo Tanzania inayo.
  • Jumuiya za kimataifa na nchi mbalimbali zimempongeza Dkt Magufuli, Rais wa Tanzania kwa kuongoza mabadiliko ya kiuchumi ambayo yameleta mafanikio katika utekelezaji wa Malengo ya Endelevu ya 2030 kama vile Elimu Bure , Kuimarisha Huduma za Afya, ujenzi wa Miundombinu na mkakati wa kuendeleza Viwanda.
Ad

Unaweza kuangalia pia

WAZIRI ZUNGU AHUDHURIA MKUTANO WA 7 WA BARAZA LA KISEKTA LA MAWAZIRI WA MAZINGIRA NA MALIASILI WA JUMUIA YA AFRIKA MASHARIKI

             

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *