NAWAHAKIKISHIA MAJI YATAFIKA KOTE NCHINI – MAKAMU WA RAIS

MAKAMU WA RAIS
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na wananchi wa kata ya Isagehe mara baada ya kukagua matanki mawili ya maji ambayo ni sehemu ya mradi wa upanuzi wa mtandao wa maji ya ziwa Victoria kwenda katika miji ya Kagongwa na Isaka kwa gharama ya shilingi blioni 24.72.
  • Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, ameendelea na ziara yake ya kukagua na kuhamasisha shughuli za maendeleo katika wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga.
SULUHU-6
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikagua matanki mawili ya maji ambayo ni sehemu ya mradi wa upanuzi wa mtandao wa maji ya ziwa Victoria kwenda katika miji ya Kagongwa na Isaka kwa gharama ya shilingi blioni 24.72.
  • Akiwa Wilayani Kahama Makamu wa Rais alitembelea mradi wa upanuzi wa mtandao wa maji ya Ziwa Victoria kwennda katika miji ya Kagongwa na Isaka wenye gharama ya shilingi bilioni 24.72 zikiwa fedha za ndani.
MATANKI
Matanki mawili ya maji ambayo ni sehemu ya mradi wa upanuzi wa mtandao wa maji ya ziwa Victoria kwenda katika miji ya Kagongwa na Isaka .
  • Akizungumza na wananchi wa kijiji cha Isagehe ambapo pamejengwa matanki mawili ya maji ambayo yana uwezo wa kubeba lita laki 8 kila moja, Makamu wa Rais alisema “Serikali ya awamu ya tano inawajali na kuwathamini wananchi wake na kuwahakikishia wananchi hao maji yatafika kote yalipoahidiwa”
MAKAMU WA RAIS
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo ya namna mazingira yatakavyoachwa mara baada ya mgodi wa dhahabu wa Buzwagi kufungwa kutoka kwa Meneja wa Mazingira na Ufungaji Mgodi Bi. Rebecca Stephen.
  • Makamu wa Rais pia alitembea mgodi wa dhahabu wa Buzwagi na kutaka kufahamu mgodi huo umejiandaaje kuyaacha mazingira salama mara baada ya kufungwa.
MAKAMU WA RAIS
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo ya namna mazingira yatakavyoachwa mara baada ya mgodi wa dhahabu wa Buzwagi kufungwa kutoka kwa Meneja wa Mazingira na Ufungaji Mgodi Bi. Rebecca Stephen.
  • Kwa upande wake Naibu Waziri Madini Mhe. Stanslaus Nyongo amesema sheria mpya ya madini itasaidia sana katika kuboresha maisha ya Watanzania wengi kwani pamoja na kodi itakayolipwa pia wachimbaji wanajukumu la kuchangia huduma za kijamii kwenye maendeo yanayozunguka mgodi.
SULUHU-1
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo ya namna mazingira yatakavyoachwa mara baada ya mgodi wa dhahabu wa Buzwagi kufungwa kutoka kwa Meneja wa Mazingira na Ufungaji Mgodi Bi. Rebecca Stephen.
  • Aidha, Makamu wa Rais aliweka jiwe la msingi la ufunguzi wa madarasa 8 ambao ujenzi wake umegharimu zaidi ya shilingi milioni 121 ikiwa ni miradi ya TEA na P4R katika shule ya Sekondari Nyashimbi wilayani Kahama.
MAKAMU WA RAIS
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasalimu wanachi wa kata ya Isaka waliojitokeza kwa wingi kumlaki wakati akiwasili wilayani Kahama kwenye ziara ya kikazi.
  • Mwisho Makamu wa Rais alihutubia wananchi wa Kahama katika uwanja wa michezo wa Taifa ambapo alihimiza wananchi hao kushirikiana na Serikali katika masaula ya maendeleo.
MAKAMU WA RAIS
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasalimu wanachi wa kata ya Isaka waliojitokeza kwa wingi kumlaki wakati akiwasili wilayani Kahama kwenye ziara ya kikazi.

Ad

Unaweza kuangalia pia

LIVE: UZINDUZI WA MAJENGO YA OFISI YA MANISPAA NA MKUU WA WILAYA KIGAMBONI JIJINI DSM

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 11, Febuari, …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *