Jengo la Uwanja wa Ndege cha Julius Nyerere Teminal Three jijini Dar es salaam ambalo Februari 28, 2019, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alikagua ujenzi wake na kuambiwa kuwa limekamilika kwa asilimia 95 na linatarajiwa kuwa limekamilika Mei mwaka huu.

UJENZI WA TEMINARL III WAFIKIA ASILIMIA 95

WAZIRI MKUU
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiaga wakati alipoondoka kwenye Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere Terminal Three, jijini Dar es salaam baada ya kukagua ujenzi wa uwanja huo ambao umekamilika kwa asilimin 95 na unarajiwa kukamilika Mei mwaka huu. Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu na TAAA
  • Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ametembelea mradi wa ujenzi wa jengo la tatu la abiria katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) na kusema ameridhishwa hatua iliyofikiwa.
TERMINAL III
Jengo la Uwanja wa Ndege cha Julius Nyerere Teminal Three jijini Dar es salaam ambalo. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alikagua ujenzi wake na kuambiwa kuwa limekamilika kwa asilimia 95 na linatarajiwa kuwa limekamilika Mei mwaka huu.
  • Mradi wa ujenzi wa jengo hilo umefikia asilimia 95 na unatarajiwa kukamilika Mei 30, mwaka huu ambapo hadi sasa tayari maeneo mengi yamekamilika ikiwa ni pamoja na sehemu za abiria wanaowasili na kuondoka.
TERMINAL III
Jengo la Uwanja wa Ndege cha Julius Nyerere Teminal Three jijini Dar es salaam ambalo Februari 28, 2019, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alikagua ujenzi wake na kuambiwa kuwa limekamilika kwa asilimia 95 na linatarajiwa kuwa limekamilika Mei mwaka huu.
  • Waziri Mkuu ambaye ametembelea mradi huo (Alhamisi, Februari 28, 2019) amesema amefurahi kukuta michoro ya wanyama kama tembo, twiga, bahari, minazi na majahazi ambayo ni alama za nchi.
WAZIRI KUU
Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akiangalia aina ya viti vya abiria vitakavyotumika kwenye Jengo la tatu la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) alipotembelea. Kulia kwa Waziri Mkuu ni Bi. Sophia Mjema, Mkuu wa Wilaya ya Ilala na wa pili kushoto ni Mhandisi Julius Ndyamukama, akifuatiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda.
  • Kufuatia kukamilika kwa uwanja huo kwa asilimia 95, Waziri Mkuu ameitaka Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) ianze kukamilisha  taratibu za kuutumia uwanja huo ili mkandarasi anapoukabidhi uanze kutumika.
WAZIRI MKUU
Kiongozi Mkuu wa Timu ya Wataalam wa Ujenzi wa Jengo la Tatu la Abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Mhandisi Julius Ndyamukama (aliyenyoosha mkono) akimuonesha Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa ukumbi wa abiria wanaoondoka katika jengo la tatu la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA)
  • Kadhalika, Waziri Mkuu ameipongeza kampuni inayojenga uwanja huo kwa kazi nzuri waliyoifanya kwa sababu jengo ni zuri na linavutia. Pia amewapongeza Watanzania wanaofanya kazi kwenye mradi huo.
WAZIRI MKUU
Waziri Mkuu Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akimsikiliza Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), Mhandisi Patrick Mfugale akisoma taarifa ya Ujenzi wa mradi wa Jengo la Tatu la Abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), leo alipowasili kukagua maendeleo ya ujenzi huo.
  • Awali, akisoma taarifa ya mradi huo, Mkurugenzi wa Walaka wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mhandisi Patrick Mfugale alimuelezwa Waziri Mkuu kuwa jengo hilo umekamilika kwa asilimia 95.05, ambapo eneo la maegesho ya ndege linaweza kuegesha ndege 19 za darala C, na 11 daraja E na jengo linaweza kuhudumia abiria 2,800 kwa saa muda ambao abiria ni wengi.
TERMINAL-A
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua kazi ya umaliziaji wa ujenzi wa Uwanja cha Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Teminal Three jijini Dar es salaam, Februari 28, 2019. Ujenzi wa uwanja huo umekamilika kwa asilimia 95 na unatajiwa kukabidhiwa kwa serikali Mei mwaka huu.
  • Mhandisi Mfugale amemhakikishia Mhe,. Majaliwa kuwa ujenzi huo utakamilika kwa wakati na kwa viwango vilivyowekwa, na kwamba jengo hilo litakabidhiwa kwa serikali tarehe 31 Mei, 2019.
TERMINAL-1
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua kazi ya umaliziaji wa ujenzi wa Uwanja cha Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Teminal Three jijini Dar es salaam. Ujenzi wa uwanja huo umekamilika kwa asilimia 95 na unatajiwa kukabidhiwa kwa serikali Mei mwaka huu.

Ad

Unaweza kuangalia pia

RAIS DKT MAGUFULI AWAAPISHA VIONGOZI ALIOWATEUA HIVI KARIBUNI KATIKA HAFLA ILIYOFANYIKA IKULU

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 03 …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *