MAABARA ZA NYUKLIA KUWEZESHA TZ KUUZA BIDHAA NJE YA NCHI POPOTE DUNIANI

  • Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania kujenga Maabara katika Kanda.
  • Maabara za Nyuklia  Mkombozi wa Mkulima, Mfugaji na Mvuvi
  • Wafanyabiashara watakiwa kuchangamkia uwekezaji wa maabara za Nyuklia.

 

  • Ili Tanzania ifanikiwe kuwa na vigezo hitajika vya kuuza bidhaa zake nje ya nchi bila kuchagua baadhi ya masoko inatakiwa kuwa na Maabara za Nyuklia zinazohifadhi vyakula na bidhaa zinazoharibika haraka.
  • Akitoa maelezo ya kina ya unzishwaji wa maabara hizo katika Kanda kwa Idara ya Habari Maelezo, wiki iliyopita, katika Ofisi ya Kanda ya Tume hiyo, zilizopo Jengo la iliyokuwa Wizara ya Elimu na Ufundi Jijini Dar-es-salaam, Mtendaji Mkuu wa Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania-TAEC Profesa Lazaro Busagala amesema;
  • “Bila kuwa na maabara za uhifadhi wa bidhaa zinazoharibika haraka tunawavunja moyo wakulima na wafanyabiashara na kuwakosesha masoko mengi ya nje, ambapo moja ya kigezo kikubwa kabisa kitakachowapa uhuru wa kuuza popote duniani ni pale vyakula na bidhaa zao  zinapoingizwa katika maabara za nyuklia”.Screen Shot 2019-03-04 at 16.10.00
  • Aidha, chakula au bidhaa inayopita katika maabara ya nyuklia ni salama zaidi kuliko bidhaa au vyakula vinavyoongezewa muda wa kuishi kwa kutumia kemikali au kwa kiingeraza presevatives ili kuzuia uharibifu, kuoza kwa chakula au bidhaa husika.
  • Hivyo, tunatumia  technolojia  ya  nyuklia  kupitisha  vyakula   kwenye  mionzi  na  kuondoa  vitu vinavyoweza  kusababisha   kuharibika   kwa  haraka,  pamoja  na  kiasi  cha  wadudu  ambao huharibu  vyakula. Hii inawezesha  bidhaa na vyakula hivyo kukaa  kwa  muda  mrefu  zaidi. Amesema Prof. Busigala
  • Akionyesha masikitiko Prof Busigala amesema kuwa hakuna Mtanzania asiyejua tatizo la upotevu wa  mazao ya kilimo wakati wa kuvuna  shambani , kusafirisha, kuhifadhi na wakati wa mazao yakiwa sokoni kwa jili ya kuuzwa, kuna asilimia takriban 40 (takwimu SUA) ya mazao hupotea. Hivyo maabara za nyuklia itasaidia kwa kiasi kikubwa  kuondoa kabisa tatizo la kukimbizana na soko kwa kuhofia  kuharibika au kuoza kabla ya kumfikia mlaji.
  • Tunachofanya  katika maabara hizi ni  upimaji  wa  kiasi cha  mionzi  inayofaa  kutumika katika bidhaa au vyakula, kuangalia muda sahihi wa kuingiza mionzi, pamoja  na kuhakikisha  wadudu   wanaoharibu wamedhibitiwa ili  kuhakikisha  usalama  wa  vyakula na bidhaa hizo na kuziacha katika ubora wake kukidhi haja ya soko.Screen Shot 2019-03-04 at 16.13.00
  • “Watu  wengi  sana  wanahusisha  nyuklia  na  vitu  vya  silaha hususan za milipuko  hatari kama mabomu, lakini ifahamike kuwa  karibu  teknolojia  zote  duniani  ni hatari, ila ndio maana Tume ipo kwa ajili ya kuhakikisha  matumizi salama ya mionzi kwa faida na kujiletea maendeleo,   kwahiyo  mionzi ya nyuklia  haibaki kwenye  vyakula  wala bidhaa husika’.
  • Mfano tunashauriwa kuota jua la saa nne kwa kuambiwa utapata vitamin D hii ina maana mionzi ya jua ya saa nne ni salama kwa afya ya binadamu. Pia, katika suala zima la Nguvu za Atomiki kuna mionzi ya Nyuklia ambayo ni salama kama hiyo inayotumika kuweka vyakula na bidhaa salama kwa kupenyeza mionzi inayouwa visababishi vya uharibifu wa vyakula na bidhaa haraka zaidi. Amesema Prof Busigala.
  • Profesa Busagala ameongeza kwa kusema kuwa zaidi ya nchi 60 duniani zinatumia maabara hizi na kuwa huru kuuza bidhaa zao popote duniani. Kwa kuwa Shirika la Biashara la Duniani – (World Trade Organization- WTO) linaelekeza uwepo maabara hizi na upatikanaji wa masoko popote duniani bila kuwa na shaka na bidhaa au chakula husika. Kwa  kuwa  inafahamu ubora na usalama wa bidhaa na vyakula vilivyopita katika maabara ya nyuklia.
  • Akitoa mfano Mtendaji Mkuu wa TAEC ameongeza kwa kusema kuwa kuna matunda mengi tunayapata kutoka Afrika ya Kusini kama Apples ambazo zinahimili kukaa katika masoko kwa muda mrefu, hii inatokana na kupita katika maabara za nyuklia ambazo zina uwezo wa kuzuia vinasaba vya uharibifu na kuleta hali ya uozo kwa tunda hilo.Screen Shot 2019-03-04 at 16.17.29
  • Akionyesha uzoefu wa TAEC katika utafiti mdogo uliofanywa Mkoa wa Arusha ambao una wakulima wengi wanaozalisha mbogamboga, matunda na maua kwa kutumia Nyumba Kitalu Prof. Busigala amesema kuwa wanazalisha kwa wingi lakini wanategemea huduma ya uhifadhi na usafiri kutoka nchi jirani.
  • ‘Hii sio sahihi kabisa, maana hatuwatendei haki wakulima na wafanya biashara wetu, hivyo,  tukaona ni vema kujenga maabara hizi katika Kanda kulingana na uzalishaji na mahitaji ya wakulima. Pia, hii ni katika kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt  John  Pombe  Magufuli aliyewekeza katika ununuzi wa ndege  za Shirika la Ndege la Tanzania –ATCL  lazima tufanikishe upelekaji wa bidhaa na vyakula vyetu katika masoko ya nje. Amesisitiza Prof. Busigala
  • Maabara hizo zitajengwa katika Kanda za Mashariki Dar-es-salaam, Unguja Kanda ya Tanzania Visiwani – Zanzibar, Dodoma Kanda ya Kati Mwanza kanda ya Ziwa, Mbeya Nyanda za Juu Kusini, Ruvuma Kanda ya Kusini na Kanda ya Magharibi Tabora na maeneo mengine yatakayopendekezwa.
  • Akielezea hasara za kusafirisha bidhaa au vyakula ambavyo havijapita katika maabaa ya nyuklia amefafanua kuwa, unaweza kusafirisha bidhaa yako ikifika uliko kusudia na kutambuliwa kuwa ina magonjwa, itateketezwa na nchi kuonekana haiko makini katika kuzingatia sheria za Kimataifa za WTO. Kwa kuwa ndio chanzo kikubwa cha kusambaza magonjwa kutoka nchi moja kwenda nchi nyingine.Screen Shot 2019-03-04 at 16.25.24
  • Aidha, inapodhibitika nchi yako imesambaza ugonjwa kutokana na bidhaa au chakula ulichosafirisha nchi inaingiza katika orodha ya kufungiwa na mpaka irejeshwa katika orodha ya kukubalika soko la kimataifa  itapata katika  mlolongo wa muda mrefu na uhakiki mkubwa.
  • Zipo nchi nyingi duniani ambazo hazipokei bidhaa au vyakula vyovyote ambavyo havijapitia kwenye maabara za nyuklia, hivyo unapokosa maabara hizi umejifungia masoko muhimu duniani. Pia, yapo masoko ambayo hayajali vigezo hivyo kwa kuwa wao sio wazalishaji, wafugaji au wakulima hususan nchi zenye jangwa kama Uarabuni.
  • Akitoa wito Profesa Busigala amehimiza wafanyabiashara kushirikiana na TAEC kwa pamoja waweze kuwekeza kwa kujenga maabara hizo ambazo ni hitaji kubwa kwa biashara zenye uhakika wa soko duniani.
  • ‘Nawaahidi  wafanyabiashara hawatajutia kuwekeza katika maabara za nyuklia kwa kuwa wakulima, wafugaji na wavuvi wetu wamehangaika kwa muda mrefu kutafuta masoko ya uhakika  ambayo yana vigezo vingi ambavyo karibu vingi vinakamilishwa katika maabara ya nyuklia’.
  • Technolojia   ya  nyuklia  inamalengo  ya  kuleta  matokeo chanya   kwa   wakulima   kwa  kupunguza  hasara  wanazozipata  kutokana  na  kuuza  mazao  yao  kwa  bei  ya chini  au ndogo kwa kuhofia kuharibika au kuoza,  bei ambayo  haikidhi  gharama walizotumia  wakati  wa  kuzalisha bidhaa au vyakula husika.
  • Akielezea majukumu ya Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania Prof. Busagala  amesema,   Tume ina majukumu ya  kudhibiti  matumizi   salama  ya  mionzi   kwa   kuhakikisha inakagua na  kutoa  leseni  ya  vyanzo vya mionzi.
  • Tume inahakikisha taratibu  za  kiusalama  na  taratibu  zake  zinatekelezwa  ikiwa ni pamoja  na  kuhamasisha  matumizi salama   ya   sayansi ya teknolojia  ya   nyuklia kwa  kufanya  utafiti  pamoja  na  kushauri Serikali,  pamoja  na  ujenzi  wa  maabara za nyuklia.
  • Tume ya  Nguvu  za  Atomiki Tanzania,   tayari   ina maabara 10 ambazo sio za bidhaa za vyakula,  miongoni   mwa   hizo 10 ni pamoja na maabara   ya  kudhibitisha  viwango  vya  mionzi   ili  wataalamu wanapokwenda  kupima  vifaa vinavyotumia mionzi  nje  kama vile hospitalini,  waweze  kupata  vipimo sahihi.
  • Maabara   ya  kupima vyakula,  maabara   ya   kupima sampuli ya mazingira,   pamoja na   maabara   ya   kupima   viwango   vya   mionzi   ambavyo   inawapa   wataalamu  muelekeo sahihi wa kifaa kilichokusudiwa.
  • Mfano Vifaa vyote vilivyopo Hospitalini vyenye kutumia mionzi ni lazima vikaguliwa na TAEC na kutibitisha usalama wake katika matumizi, kama vile mashine za Ex ray. city scan na zilizopo Hospitali ya Ocean Road zinazotoa mionzi kwa wagonjwa wa saratani.
  • Narejea tena wito wangu kwa wafanyabiashara  ambao wanapenda kuwekeza katika suala zima la maabara za nyuklia wafike TAEC, Tume itawapa kila msaada ili kufanikisha uanzishwaji wa maabara hizi ambazo ni uwekezaji mzuri na unalipa, nina hakika kupitia maabara hizi Tanzania ya uchumi wa kati utafikiwa 2025. Amesisitiza  Prof Busigala.
  • Nina hakika wakulima wetu na wafanyabiashara wenye kiu ya kupata masoko ya uhakika ya Kimataifa hawataona shida kulipa fedha kwa alili ya vyakula na bidhaa zao zinazoharibika haraka katika maabara ili kuwa na uvumilivu wa muda mrefu na kuweza kuuza sehemu mbalimbali duniani. Bidhaa ambazo zinaweza kuhifadhiwa katika maabara hizo ni pamoja na bidhaa za vyakula za kilimo, bidhaa za mifugo, bidhaa za samaki na bidhaa za mapambo kama maua. Na Judith Mhina-MAELEZO
Ad

Unaweza kuangalia pia

TANZANIA YATAKA AMANI KUPUNGUZA MZIGO WA WAKIMBIZI AFRIKA

Tanzania imetaka Umoja wa Afrika na Jumuiya za Kimataifa kuongeza jitihada na nguvu katika kuleta …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *