ENG.MFUGALE – UWANJA TUNAOJENGA DODOMA UTAKUWA NA UWEZO WA KUCHUKUA WATAZAMAJI 85,000 NA 100,005

  • Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 13 Machi, 2019 amekutana na kufanya mazungumzo na Ujumbe wa Urusi ulioongozwa na Mjumbe Maalum wa Rais wa Urusi katika masuala ya Afrika ambaye ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Mhe. Mikhail Bogdanov, Ikulu Jijini Dar es Salaam.
  • Mhe. Rais Magufuli amemshukuru Rais wa Urusi Mhe. Vladimir Putin kwa ushirikiano na uhusiano mzuri kati ya Tanzania na nchi hiyo na amemhakikishia kuwa Serikali anayoiongoza inatambua umuhimu wa uhusiano huo na kwamba itauendeleza na kuukuza zaidi hususani katika masuala ya biashara, uwekezaji, utalii na utoaji wa huduma za kijamii kama vile afya, elimu na miundombinu.
RAIS MAGUFULI
Rais Dkt John Magufuli Akiagalia mfano wa uwanja wa mpira utakaojengwa Dodoma, Uwanja mkubwa wa mpira wa miguu ambao utakaojengwa kwa ufadhili wa Mfalme wa Morocco Mohamed VI.Uwanja huo utakuwa na uwezo wa kuchukua watazamaji 85,000 (normal capacity)
  • “Naomba ufikishe ujumbe wangu kwa Mhe. Rais Putin kuwa Watanzania wanaipenda Urusi na tunamkaribisha kuja kutembelea nchi yetu pamoja na wananchi wengine wa Urusi, tunawakaribisha pia wawekezaji waje wawekeza katika fursa mbalimbali zilizopo hapa Tanzania kwa manufaa yetu sote” Mhe. Rais Magufuli amemueleza Mhe. Bogdanov.
  • Kwa upande wake Mhe. Bogdanov ambaye amewahi kutembelea Tanzania miaka 8 iliyopita ameipongeza Serikali ya Tanzania kwa kasi nzuri ya maendeleo iliyoyapata katika kipindi kifupi na amebainisha kuwa Urusi imedhamiria kukuza zaidi uhusiano na ushirikiano mzuri uliopo kati yake na Tanzania.
Screen Shot 2019-03-13 at 17.06.13
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Mikhail Bogdanov zawadi ya Kinyago cha Mpingo kabla ya mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.
  • Mhe. Bogdanov amesema Urusi inao mpango mahususi wa kushirikiana na nchi za Afrika ikiwemo Tanzania katika kuongeza kasi ya maendeleo na kwamba hivi karibu Tanzania na Urusi zitatiliana saini makubaliano ya kuanzisha tume ya pamoja ya ushirikiano (Joint Permanent Commission – JPC) katika biashara, uwekezaji na uchumi ili rasilimali na fursa zilizopo katika pande zote zitumike kwa manufaa ya wananchi wa nchi hizo.
RAIS MAGUFULI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuonesha Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Mikhail Bogdanov picha ya Mlima Kilimanjaro ambayo alimkabidhi kama zawadi kabla ya mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.
  • Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi amesema mazungumzo hayo yamekwenda vizuri na kwamba Tanzania inatarajia tume ya pamoja ya ushirikiano ya Tanzania na Urusi itasaidia kukuza uchumi kupitia madini, gesi na utalii hasa wakati huu ambapo Urusi imeitangaza Tanzania kuwa nchi yenye vivutio bora vya utalii duniani.
RAIS MAGUFULI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Mikhail Bogdanov mara baada ya mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.
  • Mazungumzo hayo yamehudhuriwa na Balozi Tanzania nchi Urusi Mhe. Mej Jen. Mstaafu Simon Mumwi na Balozi wa Urusi nchini Tanzania Mhe. Yuri Popov.
  • Wakati huo huo, Mhe. Rais Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na timu ya wataalamu wa Tanzania na Morocco wanaoshughulikia ujenzi wa uwanja wa michezo katika Jiji la Dodoma, unaotarajiwa kujengwa kwa msaada wa Mfalme wa Morocco Mtukufu Mohammed VI.
RAIS MAGUFULI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Mikhail Bogdanov ambaye aliambatana na ujumbe wake Ikulu jijini Dar es Salaam
  • Balozi wa Morocco hapa nchini aliyeongoza ujumbe wa wataalamu kutoka Morocco Mhe. Abdelilah Benryane amesema pamoja na kuzungumzia uhusiano mzuri wa Tanzania na Morocco wamejadiliana kuhusu utekelezaji wa miradi iliyokubaliwa wakati wa ziara ya Mfalme wa Morocco hapa nchini mwaka 2016 ikiwemo ujenzi wa Msikiti wa Baraza la Waislamu Tanzania (BAKWATA) unaojengwa Jijini Dar es Salaam na kuanza kwa ujenzi wa uwanja wa mpira wa miguu Jijini Dodoma.
RAIS MAGUFULI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia Kitabu chenye Mambo ya Urusi alichopewa zawadi na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Mikhail Bogdanov Ikulu jijini Dar es Salaam.
  • Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mhandisi Patrick Mfugale amesema uwanja huo utajengwa jirani na eneo la Nanenane kando ya barabara ya Dodoma – Morogoro, utajengwa kwa mfano wa mlima Kilimanjaro na utakuwa na uwezo wa kuchukua watazamaji kati ya 85,000 na 100,005.
Ad

Unaweza kuangalia pia

RAIS MAGUFULI ATEMBELEA DAR ES SALAAM ZOO, AVUTIWA NA WANYAMA WENGI WANAOFUGWA HUMO

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *