MIRADI 1,659 YA MAJI YAKAMILIKA

Huduma za Maji Mijini na Vijijini:

  • Miradi 65 imekamilika na kufanya jumla ya miradi yote iliyokamilika kufikia 1,659 na vituo vya kuchotea maji kuongezeka hadi 131,370 na kuhudumia wananchi 25,359,290.
  • Upatikanaji wa huduma za maji Jijini Dar es Salaam umefikia asilimia 85, katika mikoa mingine asilimia 80, miji midogo asilimia 64 na vijijini asilimia 64.8. Aidha, utekelezaji wa miradi ya maji katika maeneo mengine unaendelea katika hatua mbalimbali ikiwa ni pamoja na mradi wa maji wa Ziwa Victoria – Igunga – Nzega na Tabora, mradi wa maji katika jiji la Arusha na Same – Mwanga – Korogwe.
  • Vile vile, utekelezaji wa mradi wa maji katika miji 28 wenye thamani ya Dola za Kimarekani Milioni 465 upo katika hatua za kumpata Mtaalamu Mwelekezi na Mkandarasi wa mradi.
Ad

Unaweza kuangalia pia

TRA – WAFANYABIASHARA MSIJIHUSISHE NA BIASHARA ZA MAGENDO

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imewataka wafanyabiashara na wachuuzi wanaoishi jirani na fukwe za Bahari …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *