MRADI WA UMEME WA STIEGLER’S GORGE WAKAMILISHA UJENZI WA MIUNDOMBINU WEZESHI

Mapendekezo ya Serikali ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa na ya Kiwango na Ukomo wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka 2019/20,Upande wa Mradi wa Kufua Umeme wa Maji Rufiji – MW 2,115:

  • Hatua iliyofikiwa ni: kupatikana kwa mkandarasi wa mradi wa kufua umeme utokanao na nguvu ya maji katika Mto Rufiji ambaye ni Kampuni ya Ubia kati ya Arab Contractors na Elsewedy Electric S.A.E kutoka Misri ambapo mkataba wa ujenzi umesainiwa na mkandarasi alikabidhiwa eneo la mradi mwezi Februari 2019.
  • Mafanikio yaliyopatikana ni pamoja na ukamilishaji wa ujenzi wa miundombinu wezeshi ikijumuisha njia ya umeme wa msongo wa kV 33 kutoka Msamvu hadi eneo la mradi; mifumo ya huduma ya maji na ya mawasiliano ya simu; kukamilika kwa ujenzi wa nyumba 10 na kuendelea na ukarabati wa nyumba 28 za iliyokuwa kambi ya RUBADA; ujenzi wa barabara za Kibiti – Mloka – Mtemere – Matambwe Junction – Mto Rufiji (km 210) na Ubena Zomozi – Mvuha – Kisaki – Mtemere Junction (km 178.39) zimekamilika.
Ad

Unaweza kuangalia pia

SPIKA WA BUNGE AZINDUA JENGO LA MAHAKAMA WILAYA YA KONDOA

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai (Mb) leo azindua …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *