HOSPITALI YA UHURU YAUNGANISHWA NA MKONGO WA TAIFA WA MAWASILIANO

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, (iliyokuwa Sekta ya Mawasiliano), Dkt Jim Yonazi akikagua uingizaji wa fibre za Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano katika Hospitali ya Uhuru Wilayani Chamwino jijini Dodoma, jana.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari iliyokuwa Sekta ya Mawasiliano, Dkt Jim Yonazi ametembelea na kukagua hatua iliyofikiwa ya  ujenzi wa miundombinu ya Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano katika hospitali ya Uhuru inayojengwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino, jijini Dodoma

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, (iliyokuwa Sekta ya Mawasiliano), Dkt Jim Yonazi akikagua uingizaji wa fibre za Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano katika Hospitali ya Uhuru Wilayani Chamwino jijini Dodoma, jana kulia ni Meneja wa TTCL Mkoa wa Dodoma Simon Marwa.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari iliyokuwa Sekta ya Mawasiliano, Dkt Jim Yonazi ametembelea na kukagua hatua iliyofikiwa ya  ujenzi wa miundombinu ya Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano katika hospitali ya Uhuru inayojengwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino, jijini Dodoma

Ad

Dkt Yonazi amekagua Ujenzi wa wa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano, vyumba maalumu ambavyo mifumo ya TEHAMA itafungwa na kuunganishwa na Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano pamoja na  upatikanaji wa huduma za mawasiliano ya sauti na data ikiwemo mitandao ya simu za mkononi

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, (iliyokuwa Sekta ya Mawasiliano), Dkt Jim Yonazi akizungumza timu aliyoambatana nayo katika kukagua uingizaji wa fibre za Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano, vyumba vitakavyowekwa mifumo ya TEHAMA, pamoja na upatikanaji wa mawasiliano ya simu za mkononi na data katika Hospitali ya Uhuru Wilayani Chamwino jijini Dodoma, jana.

Dkt. Yonazi amesema kuwa lengo la kufanya ukaguzi huo ni kuhakikisha kuwa huduma bora za mawasiliano katika hospitali hiyo zinapatikana na zinazingatia  matumizi ya kisasa ya TEHAMA

“Jukumu letu la msingi ni kuwezesha sekta mbalimbali kutumia TEHAMA ikiwemo Sekta ya Afya, lengo ni kuhakikisha Sekta ya Afya inatumia TEHAMA katika kutoa huduma zake kwa wananchi ikiwemo elimu ya afya kwa njia ya mtandao”, amesisitiza Dkt Yonazi

Naye Meneja wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) Mkoa wa Dodoma, Simon Marwa amesema kuwa ujenzi wa miundombinu hiyo umefikia kiwango cha asilimia 60 na utakamilika na kuwa tayari kutumika mara hospitali hiyo itakapoanza kutoa huduma.

Meneja wa TTCL Mkoa wa Dodoma, Simon Marwa akitoa maelezo kwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, (iliyokuwa Sekta ya Mawasiliano), Dkt Jim Yonazi wakati alipotembelea kukagua uingizaji wa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano katika Hospitali ya Uhuru Wilayani Chamwino jijini Dodoma, jana. (Picha na WUUM

Na Faraja Mpina  (WMTH)

Katika hatua nyingine Marwa amesema kuwa TTCL inajipanga kutekeleza agizo la Dkt. Yonazi la kuhakikisha huduma za intaneti zinapatikana kwa wananchi watakaofika katika hospitali hiyo pamoja huduma za kuweka na kutoa pesa mtandaoni kwa kutumia T-Pesa

Aidha, Mratibu wa Afya ya Uzazi na Mtoto wa Wilaya ya Chamwino, Neema Mlula amesema kuwa kuwekwa kwa miundombinu hiyo na mifumo ya TEHAMA katika hospitali hiyo kutawezesha utoaji wa huduma za afya, kukusanya takwimu na kuhifadhi kumbukumbu za wagonjwa

Ameongeza kuwa, mifumo ya TEHAMA itaunganishwa kwenye  vitengo nane vya hospitali hiyo ili kufanikisha utoaji wa huduma bora na kwa wakati, huku akivitaja vitengo hivyo kuwa ni wagonjwa wa nje, idara ya mionzi, maabara, kitengo cha dawa,idara ya macho, idara ya afya ya kinywa na meno, idara ya utawala na idara ya afya ya uzazi na mtoto.

Ad

Unaweza kuangalia pia

RAIS SAMIA SULUHU AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA WAZIRI WA NCHI, WIZARA YA MAMBO YA NJE YA SHIRIKISHO LA JAMHURI YA UJERUMANI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, akizungumza na kuagana na …

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.