DKT. CHAMURIHO – ACHENI KUFANYA KAZI KWA MAZOEA

Naibu Waziri Ujenzi, Eng. Godfrey Kasekenya, akisisitiza jambo kwa menejimenti ya Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi mara baada ya kuwasili kwenye ofisi za Wizara, jijini Dodoma. Wa pili kulia ni Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Eng. Dkt. Leonard Chamuriho, kulia ni Katibu Mkuu-Ujenzi, Arch. Elius Mwakalinga na kushoto ni Kaimu Katibu Mkuu Uchukuzi Gabriel Migire.
 

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhe. Dkt. Leonard Chamuriho amewataka watumishi wa wizara Ujenzi na Uchukuzi kufanya kazi kwa kuzingatia maadili ya kazi ili kuongeza ufanisi.

Akizungumza na menejimenti ya Sekta ya Ujenzi na Uchukuzi mara baada ya kuwasili ofisini hapo jijini Dodoma ameitaka menejimneti kuunganisha wafanyakazi wa sekta zote kufanya kazi kwa kuzingatia matokeo yanayopimika.

Katibu Mkuu-Ujenzi, Arch. Elius Mwakalinga akiwakaribisha Wizarani Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Eng. Dkt. Leonard Chamuriho na Naibu Waziri Ujenzi na Uchukuzi, Eng. Godfrey Kasekenya, mara baada ya kuwasili ofisini hapo kuanza kazi jijini Dodoma

“Jipangeni kuhakikisha kuwa Watumishi wote wanafanya kazi kwa umoja na ushirikiano ili kufikia malengo yanayotarajiwa na Serikali katika kuboresha miundombinu nchini’ amesema Eng. Dkt. Chamuriho.

Amemtaka Katibu Mkuu-Ujenzi Arch. Elius Mwakalinga na Kaimu Katibu Mkuu Uchukuzi Gabriel Migire kuhakikisha miradi yote inayoendelea ujenzi wake unakamilika kwa wakati na tija.

Kwa upande wake Naibu Waziri Ujenzi na Uchukuzi, Eng. Godfrey Kasekenya ameitaka menejimenti ya Wizara kuweka ratiba ya mara kwa mara ya kukagua miradi ili kupata taarifa ya maendeleo na kuchukua hatua mapema kwa miradi yenye changamoto.

Kaimu Katibu Mkuu-Uchukuzi, Gabriel Migire akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Eng. Dkt. Leonard Chamuriho na Naibu Waziri Ujenzi na Uchukuzi, Eng. Godfrey Kasekenya, mara baada ya kuwasili ofisini hapo kuanza kazi jijini Dodoma

Akiwakaribisha Waziri na Naibu Waziri, Katibu Mkuu Ujenzi amewahakikishia viongozi hao ushirikiano kati yao menejimenti na watumishi kwa sekta anazosimamia.

Waziri Eng. Dkt. Leonard Chamuriho na Naibu Waziri Eng. Godfrey Kasekenya walikuwa katika kikao cha kwanza cha na menejimenti ya wizara mara baada  ya kuteueliwa kuongoza wizara hiyo hivi karibini.

Unaweza kuangalia pia

SERIKALI YATOA BILIONI 3 KULIPA WATUMISHI WA AFYA WALIOSHIRIKI MAPAMBANO DHIDI YA UVIKO-19

Na WAMJW – Kibaha, PWANI.Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Mhe Samia Suluhu …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.