WAZIRI WA MADINI AKUTANA NA UONGOZI MPYA WA KAMPUNI YA TANZAM 2000

Na Greyson Mwase

Waziri wa Madini, Doto Biteko leo tarehe 20 Januari 2021 amekutana na uongozi mpya wa kampuni ya uchimbaji wa madini ya dhahabu ya TANZAM 2000 jijini Dodoma uliofika kwa lengo la kujitambulisha.

Ad

Kikao hicho pia kimeshirikisha Kamishna wa Madini, Mhandisi David Mulabwa, Mkurugenzi wa Sheria wa Wizara ya Madini, Edwin Igenge, Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Mhandisi Yahya Samamba pamoja na watendaji wengine kutoka Wizara ya Madini,Tume ya Madini na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO)

Wawakilishi kutoka katika kampuni ya TANZAM 2000 walikuwa ni pamoja na Mtendaji Mkuu, Stephen Mullowney, Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Mradi, Giancardo Volo na Andrew Cheatle.

Akizungumza katika kikao hicho Waziri Biteko ameitaka kampuni hiyo kutimiza masharti yaliyowekwa ili kuondolewa kwa hati ya makosa waliyokuwa wameandikiwa na Tume ya Madini.

Masharti hayo yalikuwa ni pamoja na kupitia na kufanya marekebisho ya mpango kazi wa uendelezaji wa mgodi huo pamoja na kuwasilisha upya, kulipa fidia wananchi wanaozunguka mgodi huo katika eneo la Katoro mkoani Geita na kupitia na kufanya marekebisho ya mkataba kati yake na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO)Awali kampuni ya TANZAM 2000 ilisaini makubaliano mwaka 2011 na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) kwa ajili ya uchimbaji wa madini ya dhahabu katika eneo la Katoro Mkoani Geita, TANZAM 2000 ikiwa na hisa asilimia 45 na STAMICO hisa asilimia 55 lakini ikashindwa kuendeleza hali iliyopelekea kuandikiwa hati ya makosa na Tume ya Madini mwaka 2019

Ad

Unaweza kuangalia pia

Mitazamo ya Uongozi ya Mhe. Ummy Ally Mwalimu katika Sekta za Afya, Maendeleo ya Jamii, na Haki za Watoto

Ummy Ally Mwalimu ameonyesha mitazamo ya uongozi yenye mwelekeo wa kujali maendeleo na ustawi katika …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *