DKT. DAMAS NDUMBARO NA NAIBU WAKE MARY MASANJA WATEMBELEA SHAMBA LA MITI BIHARAMULO

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Dkt.Damas Ndumbaro akitoa ufafanuzi na maelekezo kwa viongozi wa Taasisi za Uhifadhi kuhusu masuala mbalimbali ya kuendeleza na kuimarisha uhifadhi hapa nchini mara baada ya kutembelea shamba la Miti Biharamulo -Chato mkoani Geita. 
Kamishna Mhifadhi Misitu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Prof. Dos Santos Silayo ( kushoto) akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (kulia) kuhusu ramani inayoonesha ukubwa wa eneo shamba la Miti la Biharamulo – Chato. Katikati ni Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Ezekiel Mwakalukwa.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (kulia) akiangalia moja ya shamba la miti linalomilikiwa na mwananchi karibu na Shamba la Miti la Biharamulo lililo chini ya usimamizi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania TFS akiwa na Kamishna wa Uhifadhi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania – TFS (wa pili kutoka kulia), Mkurugenzi wa Idara ya Misitu Dkt.Ezekiel Mwakalukwa ( wa tatu kutoka kulia) na baadhi ya Maofisa kutoka TFS.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja ( katikati) akiangalia miti aina ya Misingano yenye umri wa miaka 4 iliyopandwa katika shamba la Miti Biharamulo – Chato mkoani Geita wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua maendeleo ya shamba hilo.
Ad

Unaweza kuangalia pia

Mitazamo ya Uongozi ya Mhe. Ummy Ally Mwalimu katika Sekta za Afya, Maendeleo ya Jamii, na Haki za Watoto

Ummy Ally Mwalimu ameonyesha mitazamo ya uongozi yenye mwelekeo wa kujali maendeleo na ustawi katika …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *