SMZ YAJIPANGA KUJENGA MIJI MIPYA YA KISASA KATIKA SHEHIA ZA KWAHANI, CHUMBUNI NA BUBUBU

 • Mkuu wa mkoa wa Mjini Magharibi Ayoub Mohammed Mahmoud ameelezea kuridhishwa kwake na jinsi Watanzania wanaoishi nje ya nchi wanavyotafuta na kutumia fursa zilizopo kushajihisha maendeleo ya jamii nchini
 • Akizungumza na ujumbe wa Watanzania wanaoishi nje ya nchi wakiongozwa na Mwenyekiti wa baraza la Watanzania wanaoishi nje ya nchi (TDC Global) Norman Jasson ofisini kwake Vuga, alisema kufanya hivyo kunaongeza ujuzi wa wataalamu wa nyanja mbali mbali nchini na kuimarisha utekelezaji wa mipango ya maendeleo.
Z 1-01
Mkuu wa mkoa wa Mjini Magharibi Ayoub Mohammed Mahmoud
 • Amesema Zanzibar ikiwa sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inahitaji ujuzi na utaalamu utakaochochea ufanisi wa watendaji wake kalini pia kuchapuza kasi ya maendeleo ya jamii hivyo kitendo cha Wanadiaspora hao kuleta nyumbani wataalamu na wawekezaji kutasaidia kufikia malengo ya kutoa huduma bora za jamii.
 • Akitolea mfano sekta ya ujenzi, amesema serikali imepanga kujenga miji mipya katika shehia za Kwahani, Chumbuni na Bububu Kwa nyanya ndani ya mkoa huo kwa lengo la kuwapatia makaazi wananchi wake hivyo matumizi bora ya ardhi yanahitajika kukabiliana na udogo wa ardhi kulingana na ukuaji wa idadi ya watu.
Z 2-01
Mkurugenzi Mtendaji wa BT Innovetion inajishughulisha na ujenzi wa nyumba kwa bei nafuu Bw. Felix Limburg akifatilia mkutano uliofanyika Zanzibar
 • Amesema Mkoa huu ndio wenye eneo dogo kati ya mikoa yote ya Tanzania unakabiliwa na kasi kubwa ya ukuaji wa watu wenye wastani wa asilimia 49 ya watu wote wa Zanzibar hivyo teknolojia ya kisasa inahitajika ili kujenga nyumba zenye ubora kwa gharama nafuu.
 • Aidha amewashajihisha wanadiaspora hao kutumia fursa za uwekezaji ziliopo nchini zikiwemo za ujenzi kwa kuingia ubia au kuwekeza moja kwa moja kama moja ya njia za kujiendeleza kiuchumi na kuimarisha huduma za jamii.

Z 3-01

 • Awali akizungumza kwa niaba ya diaspora wengine Mwenyekiti wa Tanzania Global Diaspora Nd Norman Jasson ameambatana na wataalamu wa kampuni inayojihusisha na ujenzi kimataifa wa BT Innovation, Mwenyekiti huyo alisema wamemua kutafuta wawekezaji katika nyanja mbali mbali za kiuchumi na kijamii ili kuimarisha uchumi wa nchi na watu wake.
 • Aidha amempongeza Mkuu huyo wa mkoa kwa mapokezi na kuahidi kuwa baraza lake litaendelea kushirikiana  na serikali zote mbili za Tanzania ili kuhakikisha Watanzania waliopo nje ya nchi wanastawisha maisha ya wenzao waliopo nchini.
Z
Mwenyekiti wa Baraza la Watanzania waishio nje ya nchi (Diaspora) Duniani Norman Jasson akizungumza katika mkutano uliofanyika Zanzibar hivi karibuni.
 • Akiwasilisha mfumo wa uwekezaji na ujenzi unaotekelezwa na kampuni ya BT Inovation, Mkuu wa kampuni hiyo Felix von Limburg ameeleza kuwa kwa kutumia mifumo na teknolojia ya kisasa ya ujenzi kuna uwezekano mkubwa wa kupunguza gharama za ujenzi na athari za kimazingira.
 • Amesema kampuni hiyo mbali ya ujenzi, hutoa ushauri wa kitaalamu kuhusu ujenzi na ipo tayari kuwekeza nchini kwa kujenga nyumba zenye ubora, gharama nafuu na kwa muda mchache kupitia teknolojia ya kisasa.
Z 6-01
Mkuu wa mkoa wa Mjini Magharibi Ayoub Mohammed Mahmoud akizungumza na katika kikao na watanzania waishio nje ya Nchi (Diaspora) Visiwani
 • Wakichangia katika mkutano huo ulioshirikisha Wakurugenzi wa Manispaa zote tatu za mkoa huo, Maafisa kutoka shirika la nyumba Zanzibar na Makatibu tawala wa Wilaya na Mkoa huo walisema iwapo taasisi hiyo itaingiza nchini teknolojia hiyo itaweza kufanikisha azma ya serikali ya Zanzibar ya kuwapatia wananchi wake makaazi bora.
Z 7-01
Mwenyekiti wa TDC Chamber Of Commerce and Industry, Chiristine Chambay akizungumza katika mkutano na Mkuu wa mkoa wa Mjini Magharibi Ayoub Mohammed Mahmoud
 • Hata hivyo walisema ili kufikia mafanikio hayo, ipo haja kwa kampuni hiyo kufanya utafiti na mawasiliano na taasisi nyengine zinazotekeleza miradi ya ujenzi wa nyumba za makaazi ili kuona namna wanavyoweza kushirikiana.
 • Ujumbe huo ambao ulikuja Zanzibar kwa mwaliko wa kampuni ya TD ya Dar es salam ambapo pamoja na kuonana na Mkuu wa mkoa, ujumbe huo ulikutana na Katibu Mkuu ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Maulid Salum na Makamo wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idi kabla ya kurudi jijini Dar es salam.
Ad

Unaweza kuangalia pia

KAMPUNI YA SIGARA TANZANIA(TCC) KUTOA MSAADA WA VIFAA MBALIMBALI KWA WATU WENYE ULEMAVU ZANZIBAR

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema kwamba utayari wa …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.