- Mkuu wa Mkoa wa Katavi Juma Homera amefanya ziara katika mgodi wa Dilifu wa wachimbaji wadogo na mgodi mkubwa wa Katavi, Kapufi mining.
- Akizungumza katika ziara hiyo mkuu wa Mkoa amewaasa wachimbaji kutumie soko ya madini lilolifunguliwa mkoani humo kuuza madini yao

- Homera ameahidi kupambana na watoroshaji wa madini ya dhahabu na mpaka sasa wamekamata watu wawili kwa kununua dhahabu kinyume cha sheria kwa wakazi wa Mkoani Katavi.
- Hata hivyo Mkuu wa Mkoa Homera amesema kuwa soko la madini limeshafanya biashara kwa kununua dhahabu gramu 238, May 23/2019,na kuongeza kuwa jambo hilo lilimfanya aanze kufatilia na kubaini kuwa dhahabu nyingi inayopatikana Mkoani Katavi inauzwa nje ya mkoa wa Katavi nakupelekea soko hilo kusuasua na kuamua kuyafanyia kazi mapungufu ya soko hilo ili kudhibiti dhahabu kuuzwa bila kufata utaratibu.

- ”Mpaka sasa soko linaridhisha na kufuatia oparesheni mbalimbali zinazoendelea Soko linaendelea kufanya kazi ya ununuzi na uuzaji wa madini na mpaka sasa gramu 6317.2 sawa na Kg 6 na Grams 317.2 yenye thamani ya shilingi milioni 519,155,127.56 zimenunuliwa kwa kipindi cha Mei na Juni 30/2019 na serikali kupata mrahaba (Royality7%) shilingi milioni 36,340,858.92 na Service levy 0.3 Tsh.milioni 1,401,718.85” alisema Homera
- Aidha Mkuu wa Mkoa amesema kuwa wanaendelea kuimarisha mifumo ya kibenki katika soko hilo na kuendelea kuwabana madalali na wanunuzi wenye leseni na wachimbaji mbalimbali ili kuhakikisha wanauza madini yao kwenye soko la mkoa huo.
Ad