WAZIRI KAIRUKI ATOA WITO KWA UONGOZI WA KIWANDA CHA GOOD WILL KUZINGATIA USTAWI WA WAFANYAKAZI WAKE

 • Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Uwekezaji nchi Mhe. Angellah Kairuki ameutaka uongozi wa Kiwanda cha kutengeneza marumaru cha GoodWill Tanzania ceramic ltd  kuzingatia ustawi wa wafanyakazi wake kwa kuzingatia kanuni na sheria mbalimbali za ajira nchini ili kuendelea kuwa mazingira mazuri ya wafanyakazi wake.
KI
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Angellah Kairuki (Mb) akiangalia namna vifungashio vya marumaru vinavyotengenezwa katika kiwanda cha kutengeneza marumaru cha Good Will kilichopo Mkuranga Mkoa wa Pwani wakati wa ziara yake kiwandani hapo.
 • Ametoa kauli hiyo alipofanya ziara yake mwishoni mwa wiki katika kiwanda hicho kilichopo katika Kijiji cha Mkiu kata ya Nyamato Wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani.
 • Waziri Kairuki alieleza kuwa, upo umuhimu wa kujali wafanyakazi katika maeneo yao ya kazi kwa kuzingatia usalama na afya mahala pa kazi ili kuondokana na mazingira mabaya yanayoweza kukwamisha uzalishaji unaotarajiwa.
KI
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Angellah Kairuki (Mb) pamoja na viongozi wa Halmashauri alioongozana nao katika ziara yake kujionea namna marumaru zinavyotengenezwa katika kiwanda cha Good Will Limited kilichopo Mkuranga Pwani.
 • “Ikiwa kiwanda kimeweza kutoa ajira zipatazo 3000 ni idadi kubwa hivyo lazima myatazame mahitaji yao na kuendelea kuzingatia sheria na haki za wafanyakazi wawapo kazini,”Alisema Waziri Kairuki.
 • Aliongeze kuwa miongoni mwa maeneo muhimu kwa wafanyakazi wenu ni kuhakikisha mnawapa mafunzo kazini ili kuongeza ujuzi katika fani mbalimbali zinazoendana na uzalishaji kiwandani hapo.
KI
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Angellah Kairuki akizungumza wakati wa kikao cha majumuisho mara baada ya ziara yake kiwandani hapo.
 • Aidha aliwataka kuendelea kuwapa motisha na kuwa na njia za ubunifu katika kuhakikisha kila mfanyakazi anakuwa mwenye ustawi na kufurahia mafanikio ya uwepo wa kiwanda hicho.
 • “Ni lazima kujali masuala ya usalama wa afya zao wawapo kazini, kujali stahiki zao, kuwapa kazi zenye staha kwa kulingana na kanuni na sheria za kazi zilizopo,”alisisitiza Waziri Kairuki
KI
Meneja Mkuu wa Kiwanda cha kutengeneza marumaru cha Good Will akizungumza jambo wakati wa kikao cha majumuisho ya ziara ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Angellah Kairuki alipotembelea kiwanda hicho Mkoani Pwani.
 • Aliongeze kuwa wafanyakazi wamechangia matokeo chanya katika uzalishaji ambapo kiwanda kinazalisha marumaru mita za eneo 40,000 mpaka 50,000 kwa siku kuwa ambapo soko la ndani ni kwa asilimia 30 hadi 40 na soko la nje ni  kwa asilimia 60 hadi  70.
 • “Kiwanda chetu kimeweza kupanua soko la marumaru kwa kuuza katika nchi za nje, kwani kwasasa kiwanda kinauza marumaru katika nchi za Kenya, Uganda, Burundi, Rwanda na Congo kwa kuzingatia ubora wa bidhaa zetu,”alieleza Figa .
KI
Baadhi ya wajumbe wa kikao walioshiriki ziara hiyo wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Angellah Kairuki (hayupo pichani) wakati wa kikao cha pamoja cha majumuisho mara baada ya kumaliza ziara yake kiwandani hapo.
 • kiwanda cha Good Will Company Limited kilijengwa mwezi Machi, 2016 na kuwekwa jiwe la msingi la ujenzi wa kiwanda hiki na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Majaliwa Kasimu Majaliwa, na kuanza uzalishaji wake mnamo Mwezi Aprili Mwaka 2017.Kiwanda kinazalisha marumaru za sakafuni (floor tiles) na marumaru za ukutani (wall tiles)  kwa saizi zote na “scating”, Katika uzalishaji wa marumaru kiwanda kinatumia malighafi tofauti tofauti ambapo 95% ni malighafi toka hapahapa Tanzania na 5% kutoka China ambazo ni kemikali.
 • Malighafi zinazotoka Tanzania ni felidisper ambayo inatoka Tanga – Handeni, Morogoro na Dodoma, nyingine ni Soap stone kutoka Dodoma na Morogoro, Magnesite kutoka Same Moshi, Udongo wa mfinyanzi (clay soil) na udongo mwekundu (red soil) kutoka Mkuranga – Pwani, Limestone kutoka Mavuji – Kilwa  na Kaolin kutoka Kisarawe Pwani. Mradi huu wa ujenzi wa kiwanda umegharimu jumla ya fedha za kigeni dola milioni 50.NA.MWANDISHI WETU – OWM
Ad

Unaweza kuangalia pia

WAZIRI KAIRUKI AWAHAKIKISHIA WAWEKEZAJI MAZINGIRA MAZURI YA UWEKEZAJI

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Uwekezaji nchini Mhe. Angellah Kairuki …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *