WAZIRI WA UJENZI KAMWELE AFANYA MAZUNGUMZO NA WACHIMBAJI WA MADINI WAKUBWA ILI KUTATUA CHANGAMOTO ZAO Matokeo ChanyA+ July 4, 2019 Taarifa Vyombo vya Habari, Taarifa ya Habari, Tanzania MpyA+ Acha maoni 1,114 Imeonekana Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Mhandisi Deusdedit Kakoko akitolea ufafanuzi baadhi ya hoja za wachimbaji wa madini zilizowasilishwa kwa Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Mhandisi Isaac Kamwele wakati wa kikao hicho kilichofanyika katika ukumbi wa TPA jijini Dar es Salaam. Naibu Waziri Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhandisi Stella Manyanya akifuatilia kikao kilichojumuisha wachimbaji wa Madini wakubwa pamoja Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Mhandisi Isaac Kamwele kilichokuwa na lengo la kusikiliza changamoto wanazozipata wachimbaji hao ili waweze kutumia bandari ya Dar es Salaam kwa asilimia 100. Baadhi ya wafanyakazi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), wizara na wachimbaji wa Madini wakiwa kwenye kikao kilichoitishwa na Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Mhandisi Isaac Kamwele ili kusikiliza changamoto wanazozipata wachimbaji hao wanapotumia Bandari ya Dar es Salaam. Baadhi ya wachimbaji wakubwa wa madini wakiwasilisha changamoto kwa Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi,wanazozipata pale wanapotumia bandari ya Dar wakati wa kikao kilichoandaliwa na Waziri huyo ili kutatua changamoto hizo ikiwemo Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania Baadhi ya wachimbaji wakubwa wa madini wakiwasilisha changamoto kwa Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi,wanazozipata pale wanapotumia bandari ya Dar wakati wa kikao kilichoandaliwa na Waziri huyo ili kutatua changamoto hizo ikiwemo Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania Ad Share Facebook Twitter Stumbleupon LinkedIn Pinterest