JAFO AONGEZA SIKU 30 UKAMILISHAJI WA HOSPITAL ZA WILAYA

  • Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo ametoa siku 30 kwa Halmashauri zote zinazoendelea na ujenzi wa Hospitali za Wilaya kukamilisha kazi zote za Ujenzi ifikapo Julai 30,2019.
  • Jafo ameyasema hayo wakati alipotembelea Hospital ya Wilaya ya Singida inayojengwa katika eneo la Ilongero na kukuta ikiwa imekamilika kwa asilimia 70.

JF 2-01

  • Jafo alisema hatua niliyoikuta hapa inaotoa picha ya  uhalisia wa kazi za ujenzi wa Hospitali za Wilaya katika Halmashauri zingine Nchini hii inaonyesha wote mmeshindwa kutumia muda uliowekwa ambao ilikua ni Juni 30.
  • “Kwa ujumla sijaridhishwa  na kuchelewa kwenu kukamilisha ujenzi sababu mnawacheleweshea wananchi huduma nimekuwa nikisikia changamoto mbalimbali zilizopelekea ucheleweshaji wa kazi hii  sasa natoa siku 30  ili kila Halmashauri ikamilishe kazi zote za ujenzi ya Hospital katika eneo lake” Alisema Jafo.
  • Mhe. Jafo aliongeza kuwa Agizo hili ni kwa Halmashauri zote zinazoendelea na ujenzi wa Hospitali za Wilaya sitegemei kusikia sababu yeyote ifikapo Julai 30 ninataka kuona Hospital hizi 67 zikiwa zimekamilika tayari kuwahudumia wananchi na kama Halmashauri ina changamoto zake huu ndio wakati  wa kuzitatua, tumieni muda huu wa nyongeza vizuri kukamilisha kazi zote zilizobakia.
JF 4-01
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo akagua vifaa vya ujenzi vilivyopo katika eneo la Ujenzi wa Hospital ya Wilaya ya Singida alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya Ujenzi wa Hospital hiyo.
  • Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe. Rehema Nchimbi amesema vifaa vyote vya ukamilishaji wa ujenzi wa Hospital ya Wilaya viko katika eneo la ujenzi hivyo kazi ya ukamilishaji itafanyika kwa haraka na ujenzi utakamilika ndani ya muda uliotolewa.
  • Naye Mkuu wa Wilaya ya Singida Mhe. Pasacas Muragiri alieleza kuwa wamejipanga kikamilifu kukamilisha ujenzi huo na amemuhakikisha Mhe. Waziri kuwa watasimamia kwa ukamilifu ili kazi hiyo ikamilike kwa viwango na muda aliongeza.
  • Waziri Jafo ameanza  ziara za kikazi  kukagua maendeleo ya ujenzi wa Hospital za Wilaya ambazo alizitolewa maelekezo kukamilika kabla ya Juni,30 2019.

 

Ad

Unaweza kuangalia pia

WAZIRI ZUNGU AHUDHURIA MKUTANO WA 7 WA BARAZA LA KISEKTA LA MAWAZIRI WA MAZINGIRA NA MALIASILI WA JUMUIA YA AFRIKA MASHARIKI

             

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *