Maktaba ya Mwezi: July 2019

VIWANDA VYOTE NCHINI SASA KUWA NA TRANSFOMA ZAO

Serikali imetoa agizo kwa mameneja wote wa mikoa wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), kuhakikisha viwanda vyote nchini vinafungiwa Transfoma mahsusi kwa matumizi ya viwanda pekee pasipo kuchanganya na matumizi ya wananchi. Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani alitoa agizo hilo jana, Julai 17, 2019 akiwa katika ziara ya kazi …

Soma zaidi »

WAJUMBE WA BODI ZANZIBAR WAIPONGEZA MLOGANZILA

Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila- imewekea mikakati mbalimbali ya kuhakikisha inaendelea kutoa huduma bora za afya kwa wananchi ikiwemo huduma za kibingwa na kibobezi. Hayo yamesemwa leo jijini Dar es salaam na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Muhimbili-Mloganzila Dkt. Julieth Magandi wakati akizungumza na viongozi wa Hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar ambao …

Soma zaidi »

WAKANDARASI MSIKUMBATIE KAZI – NAIBU WAZIRI SUBIRA MGALU

Naibu wa Waziri wa Nishati, Subira Mgalu amewataka wakandarasi ambao wanadhani hawatakamilisha ama kuchelewesha kazi ya usambazaji wa umeme  vijijini  kutokana na changamoto mbalimbali , ni vyema kazi hizo wakapatia wakandarasi wenye uwezo ili miradi hiyo ikamilike kwa wakati. Akizungumzia kazi ya kusambaza umeme vijijini katika maeneo aliyotembelea mkoani Tabora, …

Soma zaidi »

ZAIDI YA MILIONII 125 ZILIZOKUSANYWA NA WAFUGAJI, TAASISI ZA UMMA NA BINAFSI, KUSAIDIA KAYA MASIKINI NGORONGORO

Zaidi ya kiasi cha shilingi milioni 125 zimekusanywa na Wafugaji katika tarafa ya Ngorongoro wakishirikiana na Viongozi wa kisiasa na Taasisi za umma na binafsi ambazo zitatumika kuimarisha vikundi vya kuweka akiba na kukopa (Vikoba ) ili kusaidia kaya masikini kujikwamua kiuchumi. Edward Maura ni Mwenyekiti wa Baraza la Wafugaji …

Soma zaidi »

SERIKALI YATOA BILION 5.7 UJENZI WA MAABARA NA JENGO LA UPASUAJI – SIMIYU

Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto yatoa kiasi cha shilingi Bilion 5.7 kwaajili ya ujenzi wa jengo la maabara na jengo la upasuaji ikiwa ni awamu ya pili, baada yakuzinduliwa kwa awamu ya kwanza na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John …

Soma zaidi »

VIONGOZI WA MAKAMPUNI MAKUBWA 20 KUTOKA CHINA KUFANYA ZIARA NCHINI

Viongozi wa Makampuni makubwa (20) kutoka Jimbo la Zhejiang Nchini China watafanya ziara nchini tarehe 20-23 Julai 2019 kutafuta fursa za kuwekeza nchini katika sekta za mawasiliano, utalii, uzalishaji, madini, filamu. Ujumbe huo utakutana na wafanyabiashara wa Tanzania kupitia taasisi ya TPSF Katika ziara ya ujumbe wa Makampuni 20 kutoka …

Soma zaidi »

RAIS DKT. MAGUFULI AFANYA UKAGUZI KATIKA MRADI WA UJENZI WA MELI MPYA, UKARABATI WA MELI YA MV VICTORIA PAMOJA NA MELI YA MV BUTIAMA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ametoa siku 5 kuanzia leo tarehe 16 Julai, 2019 kwa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano na Wizara ya Fedha na Mipango kuhakikisha vifaa vya ujenzi wa chelezo ya kujengea meli na vifaa vya ukarabati wa meli vilivyokwama …

Soma zaidi »

KIVUKO CHA MV. KITUNDA KIMEONDOA USUMBUFU WA USAFIRI KWA WAKAZI WA LINDI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amepewa pongezi na Wakazi wa Mkoa wa Lindi kwa kuwaletea huduma ya kivuko cha MV Kitunda kinachofanya safari zake kutoka Lindi kwenda ng’ambo ya pili katika eneo la Kitunda. Pongezi hizo zimetolewa hivi karibuni wakati Maafisa Habari wa Idara …

Soma zaidi »