Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete amesema kuwa Kero ya masoko ya Asali sasa imekwisha rasmi baada ya kuwaunganisha wafanyabiara asali na mnunuzi,ambapo amepatikana mnunuzi ambaye ameahidi kununua asali yote inayozalishwa jimboni humo, na kuwapatia mizinga ya nyuki na vifaa vya kuvunia vya kisasa.